ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 17, 2014

LEO NDIYO MAONYESHO YA KIMATAIFA YA ELIMU YANAANZA.

Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel (Wa pili kutoka kulia) akiwaonyesha ramani ya maonyesho ya Kimataifa ya Elimu kwa wadau wa Elimu waliojitokeza kushiriki maonyesho yanayoanza Leo Desemba 17-21, 2014 katika viwanja Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel akielezea maonyesho ya Kimataifa ya Elimu yanayoanza kesho Desemba 17-21, 2014 katika viwanja Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel akiwakaribisha wagei katika ofisi za GEL.
Washiriki wa maonyesho ya Kimataifa ya Elimu waombwa kuendelea kujitokeza ili waweze kujitangaza kutokana na maonyesho hayo yanayotarajia kuanza leo Desemba 17-21 Akizungumza wakati wa kuwagawia mabanda, Mkurugenzi Wa GEL alisema bado wanazo nafasi ni vyema washiriki wakajitokeza kwa wingi.
   Hivi wewe ni mwanafunzi? Je wajua :
·Umuhimu na faida ya mchepuo au kozi unayosoma sasa?
·Fursa ya kozi mbalimbali unazoweka kusoma baada ya kuhitimu elimu yako ya sasa?
· Fani zitokanazo na elimu unayosoma au kulenga kwa sasa baada ya kuhitimu.
·Fursa mbalimbali zilizopo katika soko la elimu kwa sasa?
Yote hayo pamoja na mengine mengi…  zikiwemo taarifa za kozi mbali mbali kama Udaktari, Biashara, Nishati na Madini hususani Gesi, urubani na zingine nyingi zitapatikana kupitia maonyesho ya elimu ya kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwl. J. K Nyerere SabaSaba Dar  s Salaam.
Fahamu pia watakuwepo wauzaji na wasambazi wa vifaa mbali mbali vya elimu kama madaftari, vitabu, uniforms, laptops na kampuni za huduma ya uchapishaji n.k
Wasubiri nini? Usikose kufika katika onesho la kipekee linaloonza, leo Jumatano tarehe Desemba 17 mpaka Jumapili Desemba 2, 2014 kuanzia saa 3 asbh – 11 jioni.
Usidanganyike urafiki wa kweli zama hizi ni wa elimu tu, hivyo basi usikose kumpatia rafiki yako juu ya onyesho hili.
Pia kwa taarifa zaidi, tembelea tovuti yet www.tiee.co.tz au piga simu namba 0656 200200

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.