MAREHEMU NDUGU
CLEMENT MABINA
Mwanaume,
baba, babu, mjomba, kaka, mwana, ndugu na rafiki wa wengi
Ulikuwa mtu mwema, mkarimu, mwenye upendo na mcheshi sana!
Rafiki uliyeaminika, uliyetegemewa, muungwana na ulikuwa mkweli sana!
Mtu wa watu, jasiri uliyejitolea kwa bidii bila kuchoka- uliwasaidia wengine, hasa waliohitaji msaada zaidi.
Hukubagua itikadi, kabila, chama, dini, rangi, elimu, wala uwezo
Ulikuwa kiongozi muelewa, mchapakazi na mwenye hekima,
Yaani kwa kweli maneno pekee hayatoshi kukuelezea ulivyotugusa wengi
Binadamu sote hatuja kamilika
Ulikuwa binadamu wa kawaida tu ila pia wakipekee
Mwenye maono, upeo wa mbali na matumaini ya maendeleo kwa wote
Uliamini kwa moyo wako wote kabisa katika uhamasishaji wa uhifadhi na udumishaji wa utamaduni wa kiafrika
Picha: Wakati bado yu hai, Clement Mabina Akishirikiana na kuhamasisha
sherehe zaUtamaduni za ‘Bulabo’ ndani yaBujora , Kisesa.
|
" Shilikare omukaya atena Magaka "
" Polisi wa Nyumbani aheshimiki "
Clement ,ki-binadamu maisha yako kwa sasa yamemalizika,
lakini mwanga wako, nafsi yako na upendo wa kudumu utaangaza duniani hapa milele, katika mioyo ya wote ambao wewe uliwagusa kimaisha
Umetoweka, lakini kamwe hutasahaulika
Maana pia maandiko matakatifu yanatufariji kwa njia gani na kwa njia gani Kristo alikufa
MWAKA MMOJA
ULIOPITA, ASUBUHI KWENYE
MAZISHI YA
MAREHEMU NELSON
MANDELA
MAISHA YAKO
YALIKATWA KIKATILI NA KIAJABU
SANA
MUNGU ANAJUA
HAUKUSTAHILI KUFA KIFO CHA
AJABU HIVYO
WALE WALIOHUSIKA, MPAKA LEO, BADO HAWAJAKABILIWA
KISHERIA
Tuna mlilia na kumuomba Mungu; muona vyote na mfahamu vyote
Kila haki na ukweli kutoka kwa Mungu ujidhihirishe kwa wote
Eh Mola, wewe ni nanga, nguvu na kimbilio letu
Clement, tunakukumbuka sana!
Kwaheri mpendwa wetu
Mpaka tutakapo kutana tena
PUMZIKA
KWA AMANI
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.