Ushauri huo umetolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Dk. Raphael Chegeni (Busega) wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Mwanza, alisema kuwa baada ya uchaguzi kumalizika kila chama kifanye tathimini na kuona wapi kilikosea na kupelekea kuanguka.
“Uchaguzi huu ni fundisho kwa vyama vya siasa ambavyo vinausajili wa kudumu na vilivyoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, sasa vijitathimini ili kujirekebisha pia vijipange na kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2015,”alisema.
Akizungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa, alisema uligubikwa na kasoro nyingi na kupelekea baadhi ya maeneo kulalamikiwa na wananchi na wanasiasa kuwa kasoro hizo zililenga kuchakachua kura na washindi katika maeneo ya mijini na vijijini.
“Kwa hili viongozi na watendaji wa serikali tuwe na utamaduni wa kuwajibika kutokana na kushindwa kusimamia majukumu yanayokuwa mbele yetu, nahili lingeweza kudhibitiwa kupitia mapendekezo ya Jaji mstaafu, Joseph Warioba katika Katiba mpya ambayo yalifanyiwa marekebisho na kuondolewa,”alisema.
Dk. Chegeni alisema kuwa CCM bado kinapendwa na wananchi hivyo viongozi wa chama hicho ngazi za Taifa, Mkoa, Wilaya na Kata kuweka watu kugombea nafasi za uwakirishi wanaokubalika na kuuzika kwa wananchi badala ya kuweka wagombea wao wanaowataka jambo ambalo hupelekea kukataliwa na wapiga kura.
“Viongozi na wanaCCM , sasa tuamke tukilala nchi itachukuliwa na upinzani na tuache kuvibeza vyama vya upinzani, kuna msemo usemao ukicheka na nyani walio katika shamba lako utakuta mabua tu, hivyo ni vyema tukaanza mkakati wa kuhakikisha pale tulipo jikwa tunayafanyia marekebisho haraka,”alisema.
Akizungumzia kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14, alisema serikali ni vyema ikazifanyia kazi haraka kasoro hizo , lakini pia kuwapa watendaji jukumu la kusimamia wenye sifa na weredi ili kuepuka migogoro na kuharibu uchaguzi kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kusimamia zoezi zima la uchaguzi.
MNEC huyo, amewataka wanasiasa wenzake kujipima kama wanatosha kabla ya kuchukua uamuzi wa kugombea nafasi za uwakirishi ili kuwasaidia kupata aibu ya kushindwa katika chaguzi mbalimbali ambazo hujitokeza kugombea bila kufanya utafiti wa kina jambo ambalo ni vyema wakalifanya kwa umakini kuepuka anguko la kisiasa.
Dk. Chegeni alisema kuwa kutokana na changamoto zilizopo nchini kwa sasa ikiwemo suala la Tegeta Escrow, Uhaba wa dawa za binadamu katika Hospitali, Vituo vya afya, Zahanati na uchangiaji wa wananchi fedha za ujezi wa vyumba vya maabara katika sekondari za kata zimepelekea baadhi ya maeneo wananchi kuiadhibu CCM kwa kuinyima kura na kutoa kwa upinzani kwa hasira.
Wito wangu kwa viongozi wa Chama kuendelea kuisimamia serikali ya CCM iliyoko madarakani ili kutekelezwa kwa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 pamoja ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ili kurejesha imani kwa wananchi hali itakachukisaidia chama kushinda katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.