Press Release
Airtel yazindua ofa kabambe ya simu wakati wa msimu wa sikukuu
· Wateja kununua simu za iPhone6, Huawei na Techno kwa bei nafuu
· Vifurushi vya Muda wa maongezi, ujumbe mfupi na internet kutolewa bure
· ofa hii itadumu kwa muda wa mienzi mitatu
Airtel Tanzania leo imetangaza ofa kabambe inayoenda sambamba na kuwazawadia wateja wake wakati wa msimu huu wa sikukuu, ofa hii iliyozinduliwa rasmi leo itawawezesha wateja kununua simu za kisasa kwa bei nafuu na kupata vifurushi vya bure vya muda wa maongezi , ujumbe mfupi na internet.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa bidhaa za kisasa Bi Prisca Tembo alisema” tunayofuraha kuzindua ofa hii ya msimu wa sikukuu na kuwawezesha wateja wetu kununua simu kwaajili yao na kwaajili ya wale wanaowapenda kwa bei nafuu zaidi sokoni.
Tembo aliongeza kwa kusema “Ofa hii inaenda sambamba na dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma bora huku tukiwawezesha wateja wetu kufaidika na huduma na bidhaa zetu. Simu hizi za kisasa (yaani smart phone) zinapatikana katika maduka yetu ya Airtel nchi nzima kwa gharama kuanzia shilingi 125,000/= hadi 979,000/=. Mteja atakaponunua simu hizi atapata na vifurushi vya muda wa maongezi, sms na internet vya mwenzi mzima, ofa hii itadumu kwa muda wa mienzi mitatu.
Ofa hii si ya kukosa, hivyo Tupenda kutoa wito kwa watanzania kuchangamkia ofa hii kwa kuwa wakwanza kununua simu ya aina wanayoipenda na kufurahia huduma zetu na kuunganishwa kwenye huduma ya internet ya 3.75G .” aliongeza Tembo.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” simu tulizonazo kwenye ofa ni pamoja na iphone 6, simu za Huawei na Techno. Simu hizi za kisasa ni rahisi kutumia na zitawapatia wateja wetu uzoefu tofauti si kwa bei rahisi tu bali zimewezeshwa na techonologia ya 3G na kuwawezesha kufurahi internet ya kasi.”
Natoa wito kwa wateja kutembelea ofisi zetu na kunua simu na kuunganishwa na huduma zetu nyingi ikiwemo Airtel yatosha, Airtel Money, huduma ya internet na vifurushi vya OMG, Switch On pamoja na huduma yetu mpya ya WiFi ya nyumbani tuliyoizindua hivi karibuni aliongeza Matinde.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.