ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 3, 2014

YAMOTO BAND WAWEKA HISTORIA BUKOBA.

Salaaam....
Na Faustine Ruta, Bukoba.
BENDI inayokuja kasi hapa nchini, Yamoto Band" kundi la vijana wenye vipaji vipya usiku wa kuamkia leo imefanya kufuru ndani ya Ukumbi wa Burudani wa "Lina's Night Club" uliopo hapa Mjini Bukoba. Ambao waliimba nyimbo zao matata za 'Najuta' ya Yamoto Band na nyingine zinazounda Album zao na kuhudhuriwa na umati wa Mashabiki ndani ya ukumbi huo na kuwafanya mashabiki muda wote kuvamia jukwaa kwa Makamuzi hayo ya kufa Mtu. Yamoto Band ambao ndio kwa mara ya kwanza kuja Hapa Mjini Bukoba wakiletwa na kampuni ya Shemeji Investment kushiriana na Ibra Cadabra.
Taswiara ya Mashabiki .
Waimbaji wa Kundi zim la Yamoto Band wakilishambulia jukwaa!!
Mambo ya Yamoto Band...Vijana kazini Bukoba!
Mmoja wa Wachezaji wa Bendi hiyo akicheza mbele ya Meza kuu

Dodo Aslay akipagawisha stejini.

Nyomi!

Makamuzi mbele ya zENyomi!

Engo ndani ya burudani.

Wakali hao ambao walikuwa hawajawahi kupiga shoo yoyote ndani ya Mji wa Bukoba waliachia radha mpya ambayo ilikuwa haijawahi kupatikana kwenye Kiwanja hicho cha Maraha Lina's Night Bukoba.

Vijana hao wa kundi la Yamoto bendi lenye masikani yake TMK jijini Dar es salaam wanaotishia bendi kongwe za hapa nchini, Yamoto Band chini ya Prezidaa wake, Dodo Aslay walivamia jukwaa na kudhihirisha kuwa wamekuja kuushika muziki wa dansi hapa nchini na kuwaambia Wakazi wa Bukoba waliopata nafasi ya kuwaona live kuwa Wamakuja kufanya kazi ya kutoa Burudani yakutosha.

Baadhi ya Mashabiki waliohudhuria kwa makini wakiwaangalia Vijana Jukwaani
Mashabiki wakiwanyanyulia Mikono juu Wasamii waKundi hilo la Yamoto Band kwenye Ukumbi wa Lina's usiku wa kuamkia leo.

Mashabiki wa Yamoto Band kwenye Ukumbi wa Lina's usiku wa kuamkia leo.

Vijana hao waliwapagawisha mashabiki kwa nyimbo zao mbalimbali kama vile Yamoto, Birthday na nyingine kibao.
Mmoja wa Waandaaji wa Show hii kutoka kampuni y Shemeji Investment Mr. Jerry Maarufu kwa jina la Mc akishangaa jukwaani Vijana wanavyokamua na Mashabiki walivyounga mkono kuingia kwa Wingi katika Ukumbi huo wa Lina's Club Bukoba mjini.





Wakina dada wakichukua picha kwenye simu zao


Mzungu wa Bukoba nae hakuweza kujificha
Ayiii...

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.