ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 18, 2014

TIMU YA KABILA LA WAJARUO YAIBWAGA TIMU YA WAHAYA “WATANI WA JADI” KUWANIA MBUZI.










TIMU ya kabila la Wajaruo jana iliwabwaga watani wao wa jadi timu ya Wahaya na kujinyakulia zawadi ya Beberu la mbuzi katika pambano kali la kusisimua lililofanyika kwenye uwanja wa Magomeni Kirumba wilayani
Ilemela jijini hapa.

Pambano hilo lilioandaliwa na mdau wa soka Muzo Cremency kwa ufadhili wa Mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo (CCM) baada ya kuwepo mabishano ya muda mrefu kutoka kwa watu wa makabila yayo yenye watani wa jadi, wanaofanya shughuli zao za kila siku katika soko kuu la Kimataifa la Mwalo wa Kirumba, vijiwe vya bodaboda, kahawa, chipusi na mamalishe.

 Mpambano huo uliohudhuliwa na mgeni rasmi katika pambano hilo alikuwa Mkuu wa Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ilemela, Joyce Kotecha ambaye alialikwa kutokana na kukubalika kwake na pande zote mbil, pia mamia ya wakazi wa Kata ya Kirumba na kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.

Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa mpambano huo wa watani wa jadi aliwataka wachezaji na wananchi kushirikiana kwa kila jambo na kudumisha mira za makabila yao zisizokuwa potofu bali zenye lengo ya kuelimisha jamii na kupiga vita vitendo vya uhalifu na kuhakikisha Polisi jamii inakuwa sehemu ya usalama wao na kutojichukulia sheria mkononi kwa kufanya uhalifu.

Timu hizo hadi mapumziko zilitoshana nguvu na hazikufunga na kipindi cha pili kilishuhudia kila upande ukifanya mabadiliko ya wachezaji huku mamia ya wananchi wakiwemo wa makabila hayo ambayo ni watani wakishangilia wachezaji wao, dakika ya 35 kipindi cha pili Steven Otieno aliwainua mashabiki kwa kupachika bao malidadi.

Timu ya kabila la Wajaruo hadi dakika 90 zinamalizika ikaibuka na ushindi wa bao moja , ikiongozwa na Mbunge Airo wakikabidhiwa beberu la mbuzi ikiwa ni zawadi ya mshindi wa mchezo huo ambao ulivuta hisia za wananchi wa kila lika na jinsia za wanaume na wanawake waliofurika hushuhudia mpambano huo.

Mbunge Airo aliyedhamini matangazo ya pambano hilo alisema kuwa mchezo huo umefungua historia mpya, ameahidi kuyaboresha zaidi kwa kushirikisha timu zingne za makabila mengine ambayo ni watani ya mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchini ili pia kutoa fursa kwa vijana kuonyesha vipaji vyao vitakavyowezesha kupata timu za ligi mbalimbali kuwasajili ikizingatiwa soka ni ajira.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.