ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 20, 2014

"HAKUNA EBOLA SENGEREMA" ASEMA MKUU WA MKOA WA MWANZA

Mkuu Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akitoa taarifa ya mkoa kuhusu kanusho la kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola wilayani Sengerema "Kwa haraka haraka mgonjwa huyo aliyefariki dunia kama angekuwa wa Ebola basi matokeo yangeonekana kwani Nyumbani alipougulia mgonjwa huyo kwa watu waliokuwa wakimshughulikia kwa karibu bila kuchukuwa hatua zozote za kujikinga wapo salama mpaka leo, kijijini hata sehemu zote za mikusanyiko ndani ya Upandwa Mwangika wilayani Sengerema hakuna taarifa ya mtu yeyote aliyedhurika, madaktari waliompokea awali wote wako katika hali salama... kwa tafsiri hii mgonjwa huyo hakuwa wa Ebola ...." ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA    


Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dr. Kengia.
TAARIFA zinazosambazwa kuwa kuna mgonjwa wa Ebola kagundulika wilayani Sengerema mkoani Mwanza, si za kweli.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini Mwanza, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dr. Kengia amesema utafiti wa awali kabla ya majibu kamili ya vipimo unatosha kujidhihirisha kuwa mgonjwa aliyedaiwa kufariki dunia hivi majuzi Salome Richard (17) siyo kweli kwamba amefariki kwa Ebola.

Hata hivyo kulikuwa na uchukuaji wa vipimo vya awali ambapo, Majibu ya Vipimo vya awali yamepatikana tarehe 19/10/2014 saa 3:00 asubuhi 

VIPIMO WALIVYOPIMA 
1. Dengue fever
2. Chikungunya Virus
Majibu ya vipimo hivyo walionekana ni Hasi (Negative)

VIPIMO VINGINE VINAVYOENDELEA 
(1) Liver function - kuangalia kama ini la mgonjwa ambaye ni marehemu lilikuwa kinafanya kazi vizuri au la.
(2) Bilirubin kuangalia kiwango cha protein kwenye ini kama kilikuwa sahihi au kimeongezeka.
Taratibu zinaendelea kati ya Mkuu wa Maabara ya Taifa na Wizara ya Afya kuhusu sampuli hii kupelekwa Mbeya au jijini Nairobi nchini Kenya kwaajili ya uchunguzi wa virusi ya Ebola au Marbug.
Mkuu Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akitoa taarifa ya mkoa kuhusu kanusho la kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola wilayani Sengerema.
Mkuu Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo (katikati) amewatoa hofu wakazi wa Sengerema, Mkoa wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla kwa kukanusha taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola wilayani Sengerema. 
HAPA MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY

Baadhi ya wataalamu wa Afya mkoa wa Mwanza walikuwepo kwenye uwasilisha wa taarifa hiyo.
Sehemu ya kusanyiko la wataalamu wa Afya na waandishi wa Habari toka vyombo mbalimbali waliohudhuria utolewaji wa taarifa ya mkoa leo mchana katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Awali kutokana na hofu ya ugonjwa huo huku taarifa zisizo rasmi zikizidi kusambazwa kwa njia ya mitandao ya simu na internet wananchi wa wilaya ya Sengerema na vijiji vya karibu walihaha katika vyombo vya usafiri husussani daladala wakikataa kugusana kwa kuwa Ebola imeingia Mwanza, huku wafanyakazi na wafanyabiashara wanaoishi mkoani Mwanza na kufanya shughuli zao wilayani Sengerema wakiahirisha kuelekea wilayani humo kutokana na vitisho vya taarifa walizopata.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.