Katibu tawala wa Wilaya ya Magu, Thomas Nyansasi, akisoma hutuba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Jackiline Liana jana wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja ya TASAF awamu ya tatu. |
Ni sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama wilaya ya Magu. |
Madiwani toka kata mbalimbali za jimbo la Magu wakiwa katika warsha ya ufunguzi waTASAF awamu ya tatu. |
Wataalamu wawezeshaji wa TASAF Halmashauri ya Magu. |
Wanafunzi wa kidato cha tano na cha sitwa shule ya sekondari Magu wakiwa kwenye mstari kwaajili ya kupata lishe ya uji shuleni hapo. |
Wanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya sekondari Magu wakipata uji shuleni hapo kutoka kushoto ni Nyanda Halili, Renatus Kamani, Francisco Katura na Emmanuel Aloyce. |
Watoto wa mtaani (majina yao hayakupatikana) wakiwa na bakuli la uji baada ya kupewa kutokana na kuombaomba katika eneo hilo la shule ya sekondari Magu. |
MKUU wa Wilaya ya Magu, Jackline Liana amewataka wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III) kwa kulenga zaidi Kaya maskini na hatarishi vijijini.
Akisoma hutuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Thomas Nyansasi, katika ufunguzi wa warsha ya siku moja jana, Liana alisema kwamba endapo wataalamu wataelewa vyema na kuwafikia walengwa kutasaidia kuondoa mauaji ya watu wenye ulemavu na vikongwe maeneo ya vijijini.
Pia wataalamu wawezeshaji wanaoshiriki warsha hiyo watumie fursa ya kujadiliana kwa kina na kubadilishana uzoefu ili kuutekelezaji wa mpango wa TASAF awamu ya tatu uweze kumaliza umaskini na hali mbaya ya wananchi walioko vijijini na kusaidia watoto kupata elimu ili kuwapa mwanga wa kuondokana na hali hiyo katika familia zao.
“Mpango huu ulenge kikamilifu wananchi wanaoishi katika Kaya masikini na mazingira hatarishi kwa kuzingatia taratibu na hali halisi ya wananchi hao ili kufikia malengo yaliyowekwa na serikali ,”alisema
Liana alisema katika maeneo mbalimbali ya vijiji na mitaa ya wilaya hiyo kuna changamoto nyingi zinawakabili wananchi walio masikini na waishio katika mazingira hatarishi na kusababisha kuwepo mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) hivyo ukitekelezwa vyema utakomesha mauaji hayo.
“Mategemeo yangu kuwa utekelezaji wa mpango huu wa kunusuru Kaya maskini utaimarisha uwazi, uwajibikaji na kutoa fursa kwa makundi mbalimbali kushiriki kwa kutumia mfumo madhubuti wa kubaini walengwa katika vijiji na mitaa yetu,”alisisitiza.
Kwa upande wake Mhandisi Eliasifa Kinasha ambaye ni Meneja wa Miradi TASAF makao makuu aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TASAF makao makuu, alisema walengwa wa mpango huo ni wananchi walio katika kaya maskini na mazingira hatarishi, hususani watoto na mama wajawazito kupata lishe bora, huduma za afya na elimu.
“Tuhakikishe watoto waliochini ya miaka mitano wanahudhuria kiliniki, wanafunzi wanasoma shule za awali, shule za msingi na sekondari na mama wajawazito wakijifungua salama katika zahanati na vituo vya afya ,”alieleza.
Aidha mpango huo utawezesha wananchi kupata ajira ya muda kwa kaya maskini zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi , wakati wa kipindi cha hari na ruzuku itatolewa kwa kayo zote zilizotambuliwa na kuingizwa katika utekelezaji wa mpango huu wa TASAF awamu ya tatu.
Wito wangu kwa wataalamu wawezeshaji , madiwani na watendaji wa Kata wa Halmashauri kupitia warsha hii wataongeza uelewa katika utekelezwaji wa mpango huu katika maeneo mbalimbali yatakayobainishwa kwenye vijiji na kata katika kuwahudumia walengwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Naomi Nko akikaribisha wadau mbalimbali kwenye warsha ya siku moja ya TASAF awamu ya tatu. |
Awali kabla ya kumkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa TASAF makao makuu, Kinasha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mwl.Naomi Nnko, alisema watendaji na wataalamu watakaopata mafunzo ya utekelezaji wa mpango wa awamu ya tatu hawatachakachua na badala yake watawafikia walengwa kutoka Kaya maskini na zilizo na mazingira mazuri.
Nnko aliwataka wananchi kushiriki kuwatambua wananchi walio masikini zaidi na wanaoishi katika maingira magumu ili kuondoa malalamiko kwani wao ndiyo wanaowatambua na kuishi nao katika maeneo mbalimbali ya vijijini na mitaa ya Kata za Jimbo na Wilaya ya Magu.
"Tutazingatia zaidi changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa kutekeleza mpango huu wa maendeleo ya jamii katika awamu ya kwanza naya pili, hivyo tutahakikisha utekelezaji huu unafakikiwa kama serikali ilivyokusudia kuondoa umaskini kwa wananchi wake ili kupata huduma bora katika uboreshaji wa miundombinu kwenye sekta za Afya, Elimu, Maji na Kilimo, Uvuvi na Ufugaji sanjari na Mawasiliano na Barabara,"alisema.
Wito wa Halmashauri ni kuwaomba wananchi na wadau wa maendeleo kuungwa mkono mpango huu kwa kuhakikisha wananchi wanaelimisha zaidi kwa njia za mikutano ya hadhara ili kuweza kuwafikia walengwa na kuwezesha wananchi kuwa wawajibikaji katika maendeleo na kukuza uchumi wa taifa lao.
Meza kuu na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya wilaya ya Magu katika picha ya pamoja. |
Meza kuu katika picha ya pamoja na wataalamu wawezeshaji. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.