ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 10, 2014

WANAFUNZI 85 KATI YA 182 WALIOACHA MASOMO WILAYANI RORYA KUSAKWA NA SERIKALI: YASEMEKANA WENGI WAMEACHISHWA SHULE ILI WAOZWE

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa, Rachel Kassanda akiweka jiwe la msingi kwenye shule ya sekondari ya Roche katika tarafa ya Girango wilayani Rorya mkoani Mara.
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa, Rachel Kassanda, amewaagiza viongozi wa serikali na walimu wa shule ya sekondari ya Roche katika tarafa ya  Girango Wilayani Rorya kuwatafuta wanafunzi wa kike wapatao 85 walioacha masomo kati ya 182 waliopo shuleni hapo.


Kauli hiyo aliitoa jana wakati alipokuwa akifungua jengo la Bweni la wanafunzi wasichana, lililojengwa kijiji cha Roche kutekeleza Mpango wa Maendeleo Elimu ya sekondari (MMES) ulianza mwaka 2012/2013 wa kusaidia ujenzi wa mabweni matano ya wanafunzi wasichana ili kuwasaidia ili waweze kupata masomo wakiwa shuleni hapo.

“Haikubaliki wanafunzi 269 walioanza masomo kakika sekondari hii leo wamebaki 182 na kati ya hao waliopo shuleni ni 97 na 85 wameacha masomo kwa sababu ambazo hazieleweki hivyo nawaagiza viongozi wa serikali, walimu kushirikiana na wazazi kuhakikisha wanafunzi hao wanapatikana na kurudi kwenye masomo,”alisema.

Kiongozi huyo aliwahasa wazazi na walezi kuwaacha watoto wao wasome na kupata elimu kwani ndiyo mkombozi wa maisha yao kutokana na hali iliyopo sasa kuwa doa kwao kutokana na ukatili na udikteta wa kuwanyima masomo kwa visingizio ambavyo mwisho wa siku ni kuwafanya wawe masikini wa elimu na maendeleo.

“Tunayo mifano mingi ya wanawake waTaifa hili ambao walipatiwa elimu na kuwa viongozi wa kimataifa ikiwa ni pamoja na Balozi Getruda mongela (Katibu Mkuu wa Mkutano wa Wanawake Beinjing China), Dk Asha Rose Migiro (Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa), Prof Anna Tibaijuka (Mkurugenzi wa Makazi UN HABITAT Umoja wa Mataifa) na Anna Makinda (Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania),”alisisitiza.
Mkuu wa shule ya sekondari Happiness Alexander akisoma taarifa ya shule.
Kwa upande wake Mkuu wa Sekondari hiyo Happiness Alexander akisoma taarifa hiyo alisema wanafunzi hao wameacha masomo yao kutokana na kuozwa, kushiriki matanga kwa muda mrefu, kuacha kutokana na wengine kujiingiza kwenye vitendo vya ngono na biashara pamoja na kilimo.

Alexander alisema kuwa jengo hilo lililojengwa na Mkandarasi, Kampuni ya MS Victoria kwa gharama ya Sh milioni 98,603,000 ambalo litachukua wanafunzi 48 kati ya 97 waliopo sekondarini hapo ikiwa ni sawa na asilimia 50 ikiwa ni moja kati ya mabweni matano yaliyojengwa kwa mpango wa MMES kwa gharama ya Sh milioni 400 zilizotolewa na Halmashauri ya Rorya.
Wanafunzi wa shule mbalimbali jirani na Shule ya sekondari ya Roche wameungana katika tarafa ya Girango wilayani Rorya mkoani Mara kwaajili ya kuulaki Mwenge wa Uhuru.
Paredi la makaribisho.
Ukaguzi ukiendelea katika mabweni ya Shule ya sekondari ya Roche.
Hatua kwa hatua na ukaguzi wa bweni la wasichana.
Sehemu maalum kwaajili ya kujiswafi.
Mabafu.
Upande wa mbele wa jengo la bweni.
Wadau wa kikundi cha NYAMIDAKOLA chenye wanachama 26 kilichopo katika kijiji cha Roche tarafa ya Gilango kata ya Roche wakionesha bidhaa zao ambazo huzalisha kwaajili ya kujikwamua kiuchumi.
Bidhaa zinazotumia nishati ya mwanga wa jua ni moja kati ya midadi ya ujasiliamali inayo kuza kipato kwa kikundi cha NYAMIDAKOLA
Ufinyanzi seksheni nyingine ya kukuza kipato kwa kikundi cha NYAMIDAKOLA kijiji cha Roche tarafa ya Gilango kata ya Roche.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa, Rachel Kassanda akipata maelezo ya shughuli mbalimbali toka kwa wadau wa kikundi cha ujasiliamali na uzalishaji NYAMIDAKOLA kilichopo katika kijiji cha Roche tarafa ya Gilango kata ya Roche.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa, Rachel Kassanda akizungumza na wanakikundi kuwatia moyo na hamasa. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa, Rachel Kassanda akipokea zawadi toka kwa mmoja ya wawakilishi wa kikundi cha wajasiliamali NYAMIDAKOLA wa kijiji cha Roche tarafa ya Gilango kata ya Roche.  
Mwenge wa Uhuru pia ulifika katika Kituo cha Kilimo/Ugani cha MVIWANYA Mtandao vikundi vya wakulima na wafugaji vilivyopo katika kijiji na kata ya Nyancha tarafa ya Shirati wilayani Rorya mkoani Mara.
Wadau mbalimbali wa Mbio za Mwenge wilaya ya Rorya walipotembelea mtandao wa vikundi vya ujasiliamali wa MVIWANYA  na kununua baadhi ya bidhaa.
Manunuzi kwa vinywaji vya mvinyo aina ya Banana wine yakifanyika.
Jinsi ya kutumia nyezo ya majiko banifu yanayo saidia kudhibiti uhalibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.
Mwenge huo umekuja kuzindua miradi katika Kata na Vijiji ya Ikoma, Roche,Nyancha na utalala katika Mji wa Utegi wilayani humo ambapo ujumbe maalumu wa mwenge mwaka huu ni Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Mapambano dhidi ya Ukimwi, Maralia, Dawa za Kulevya na Rushwa uliotolewa kila na viongozi wa kitaifa wa mbio za mwenge ambapo pia waliwahamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura za maoni wakati ukirejeshwa kwao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.