OCD aliyasema hayo hivi karibuni, wakati alipokuwa akisimamia uteketezwaji wa kiasi cha tani moja za bangi, zoezi lililofanyika katika eneo maalum la uwanja wa Kituo cha Polisi Utegi. “Bangi inayolimwa Tarime na Rorya inasemekana hufadhiliwa na raia kutoka nchi ya Kenya, lakini tutaendelea kupambana ili kutokomeza biashara ya zao hilo,” alisema .
Pamoja na hayo, aliwashutumu baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi wasio zingatia maadili pamoja na baadhi ya watumishi wa Serikali, kwamba wanajihusisha na biashara hiyo haramu.
“Kuna maofisa wa polisi wasio waaminifu wanavujisha siri tunapoandaa mkakati wa kutokomeza zao hili katika Wilaya za Tarime na Rorya na hali hii inaonyesha wanahusika moja kwa moja na biashara hii,” alisema. BOFYA PLAY KUSIKILIZA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum wilaya ya Rorya kwa kutambua kuwa madawa ya kulevya ni kikwazo cha maendeleo ya wananchi hasa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa, limekuwa likiendelea kufanya operesheni katika maeneo yote yanayozunguka wilaya ili kutokomeza madawa ya kulevya hasa bangi ambayo inalimwa katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Hivyo kwa kushirikiana na wananchi kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi jeshi hilo limeendelea kupokea taarifa kutoka kwa wananchi na raia wema kuhusiana na uhalifu wa kilimo cha bangi na wahalifu wenyewe wanaoendeleza kilimo hicho haramu ndani ya wilaya ya Rorya.
Kutokana na taarifa hizo wameweza kugundua mashamba 22 ya bangi katika vijiji mbalimbali na hatimaye kuyateketeza na kuyafyekwa na kuyachoma moto.
Pia Jeshi hilo limefanikiwa kukamata wahalifu wapatao sita waliojihusisha na kilimo hicho na kuwafikisha mbele ya vyombo vyasheria ambako kesi mbalimbali zinaendelea mahakamani, na baadhi ya bangi iliyokamatwa ndiyo hii inayoonekana katika picha mtandaoni hapa ambayo rasmi imeteketezwa kwa kuchomwa moto na waandamizi wa mbio za mwenge wa uhuru waliodhuru wilayani humo kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo na kuweka mawe ya msingi kwa baadhi ya miradi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.