Na
Mwandishi Wetu.
KLABU ya Anatory ya Morogoro, Ngija
Masters ya Iringa na Break Point ya Mbeya zimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mikoa katika fainali za mashindano ya mchezo wa
Pool ngazi ya Mikoa yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa
wiki mikoani humo na kuzawadiwa kila klabu fedha taslimu Shilingi 800,000/=
pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye fainali za Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani
Kilimanjaro.
Kwa matokeo hayo ya mikoa mitatu ndipo mtanange wa kuwatafuta mabingwa kutoka katika mikoa
17 inayoshiriki fainali za mashindano ya Safari Pool 2014
unafungwa rasmi na tunaelekeza nguvu na masikio kwenye fainali za kitaifa Septemba 14
mwaka huu.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume Morogoro,
Bingwa mtetezi wa mkoa, Mussa Mkwega alitetea vyema ubingwa wake, Iringa ni Godlove Chalangwe ndiye alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa wakati Mbeya ni Majali wa Sipilian alitwaa ubingwa wa mkoa wa huo na kwa ubingwa huo kila mmoja alizawadiwa pesa taslimu Shilingi 400,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume.
Mchezaji mmoja mmoja Wanawake waliofanikiwa kutwaa ubingwa ni,
Morogoro, Bingwa mtetezi Rosemary Deus alitetea vyema ubingwa wake, Iringani Naomi
Ngede alitwaa ubingwa wakati jijini Mbeya ni Happness Robert ndie alitwaa ubingwa wa mkoa na kwa ushindi huo kila mmoja alizawadiwa pesa taslimu Shilingi
300,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa upande wa mchezaji mmoja mmoja wanawake.
Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion”
zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17
ambayo ni Tabora, Shinyanga, Dodoma
Mbeya, Iringa, Morogoro, Mwanza, Kagera, Manyara, Arusha, Tanga, Pwani, Ilala, Lindi, Temeke, Kinondoni
na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.