JUMLA ya timu 32 za kategori tofauti tayari zimethibitisha kushiriki Michuano ya Kombe la Afrika Mashariki la Alliance (Alliance East Africa Cup) yatakarajiwa kuanza kutimua vumbi ijumaa ya wiki hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika nchini Tanzania.
Uwanja ulioteuliwa kufanyika uzinduzi kwa michuano hiyo ni dimba la CCM kirumba Mwanza, nayo fainali itachezwa tarehe 27 na 28 mwezi huu Septemba 2014 katika viwanja vya Alliance Academy Mwanza vilivyo kamilika mara baada ya maboresho kufanywa kwa hisani ya shirikisho la soka nchini TFF.
Mkurugenzi wa kituo cha elimu na michezo cha Alliance Academy ya jijini Mwanza, James Bwire amevishukuru vyombo mbalimbali vya habari nchini ikiwemo Radio ya watu Clouds Fm kwa kutia hamasa kwa michuano hiyo kiasi cha kusababisha timu mbalimbali hata zile zilizo nje ya nchi kuhamasika kushiriki michuano hiyo.
Aidha wadhamini mbalimbali tayari wameanza wamejitokeza kusapoti mashindano hayo, hali ambayo imetia hamasa katika matayarisho. Zaidi Mratibu wa Mashindano ya Alliance East Africa Cup James Bwire anatiririka juu ya maendeleo ya mashindano hayo.. (BOFYA PLAY KUMSIKILIZA)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.