MASHINDANO YA DEREVA YA MWAKA YA SCANIA.
“Bingwa wa Mabingwa” – Mashindano ya dereva ya duniani.
Dar Es Salaam, Jumanne 9 Septemba 2014
Scania
Tanzania leo hii imetangaza kwamba matayarisho ya “Mashindano ya Dereva ya
Mwaka 2014 Tanzania” yamekamilika. Mashindano hayo ambayo yanatokea kila baada
ya miaka 2 itafanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Dar es
Salaam, Jumamosi tarehe 13 Septemba 2014.
Akizungumza na
waandashi wa habari, Mkurungenzi Mkuu wa Scania Tanzania Bwana Anders Friberg
alisema, “Tunafurahi sana kuanda mashindano haya kwa mara nyingine tena. Huu ni
Mwaka wa 2 kwetu sisi kuanda Mashindano haya Tanzania tangu ya Mashindano haya
yalizinduliwa 2003. Mara ya kwanza Mashindano haya kuandaliwa ni Mwaka 2011
mshindi akiwa Bwana. Erasmus Mtui, dereva wa magari makubwa kutoka kampuni ya
Super Star Forwarders. Bw. Mtui alipata fursa ya kuiwakilisha Tanzania katika
Mashindano nchini South Africa”.
Ilikushiriki
katika Mashindano haya, Scania inatuma mwaliko kwa makampuni yaliyosajiliwa
Tanzania na madereva ambao wanataka kushindana wanajisajili kupitia makampuni
yao. Mwaka huu mashindao yalianza na madereva 25 ambao walishiriki katika
nyanja mbalimbali na washindi wa kwanza wa 5 watapata fursa ya kushindana Jumamosi
hii.
Bw. Friberg
aliendelea kwa kusema, “Mashindano ya Scania- Tanzania Driver of the Year
competition” inatoa jukwa la kujadili na kushughulikia masuala ya kusaidia
kupunguza ajali za barabarani, kuongeza faida na endelevu ndani ya sekta hiyo.
Pia inaadhimisha ujuzi wa dereva na umuhimu wao katika jamii. Madereva ni uti
wa mgongo wa biashara ya usafiri na licha ya kutengeneza malori yenye ubora na
usalama zaidi, Scania pia inamzingatia dereva.
Bw. Friberg alitaja kwamba mshindi wa kwanza hadi wa tatu watapata
makombe kila mmoja na watafadhiliwa Mashindano ya kikanda Afika Kusini baadaye
Mwaka huu.
Mashindano hayo yatahudhuriwa na Kamanda wa Trafiki Mohammed Mpinga
ambaye atakuwa Mgeni Rasmi, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Balozi Lennart
Hjelmaker na Mwenyekiti wa TOTOA Seif Al Hosni.
Mashindano
ya 2014 yatatimisha mara ya 6 ya Mashindano haya ya kimataifa amabyo
ilianzishwa mwaka 2003 na ni shindano kubwa zaidi ya malori duniani.
Mashindano
haya yalianza kwa kuitikia wito wa Tume ya Ulaya ya kutoa fursa ya kuwapa
mafunzo madereva malori, kupunguza madhara ya mazingira yanayotokana na
uendeshaji malori, kuongeza usalama barabarani na kuboresha matumizi ya mafuta.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.