ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 22, 2014

KATIBU WA TFF AIPONGEZA ALLIANCE KWA KUIBUA VIPAJI VYA VIJANA KATIKA SOKA NA WAAMUZI BORA WA BAADAE

Mwaamuzi bora wa mashindano ya Kombe la Meya 2014, David Albert, mwanafunzi wa darasa la tano wa shule na kituo cha Elimu na Michezo cha Alliance akiwapungia mikono wadau wa michezo na wananchi waliofurika uwanja wa michezo wa Nyamagana baada ya kumalizika mchezo wa fainali baina ya timu za Kata za Mkolani na Milongo na bingwa kuibuka Mkolani kwa bao 2-1 aliyochezesha. 
NA PETER FABIAN, MWANZA.

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine, amekunwa na Kituo cha Elimu na Michezo cha Alliance cha jijini Mwanza kwa kuanzisha mpango wa kuanda vijana wadogo kuwa waamuzi bora wa soka mkoani na nchini hapa.

Selestine alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Mwanza, wakati alipohudhulia mchezo wa fainali za mashindano ya Kombe la Meya 2014 katika uwanja wa Nyamagana baina ya timu Kata ya Mkolani FC na Kata ya Mirongo FC ambapo Mkolani ikiwachapa kwa ushindi wa bao 2-1 na kunyakuwa ubingwa wa mwaka 2014.

“Nitumie fursa hii kuupongeza uongozi wa Kituo cha Alliance kwa kuendeleza vijana katika tanisia ya michezo mbali ya kuwapatia mwanga wa elimu lakini kuhakikisha Sekta ya michezo inaendelezwa ikiwa ni sera ya Taifa,”alisema.

Katibu huyo alisema Kituo cha Alliance ambacho kinamilikiwa na Kampuni ya Nyamwaga chini ya Mkurugenzi wake James Bwire kimekusudia kuondoa uhaba wa waamuzi kwa kuanzisha mafunzo kwa vijana wadogo ambao tumeanza kuwashuhudia waamuzi wake wakichezesha mashindano ya kombe la Meya 2014 kwa kiwango bora.

“Tunalo tatizo kubwa la waamuzi nchini lakini kwa mpango huu nadhani mbeleni litakuwa limemalizika kwa kuwa Alliance imeanza kutekeleza jukumu hilo ambalo nimeambiwa kuwa liko chini ya mwamuzi mstaafu wa kimataifa aliyewahi kuwa na beji ya FIFA ambaye ndiye mkufunzi wa vijana hawa Alfred Rwiza, nimpongeze kwa juhudi anazozifanya,”alisisitiza.
Diwani wa Kata ya Mirongo, Daudi Mkama (CUF) kushoto mbele, akimkabidhi zawadi ya Sh laki mbili, David Albert, kulia wa Kituo cha Alliance kwa kuwa  mwaamuzi bora wa mashindano ya Kombe la Meya 2014 yaliyomalizika wiki iliyopita katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. Katikati aliye vaa jaketi la blue akitabasamu ni Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine na nyuma kulia ni mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo.
Selestine alieleza kuwa TFF inatakiunga mkono wa dhati Alliance kwa kuwa kituo bora cha kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana ili kufikia malengo ya Taifa, pamoja na kuhakikisha waamuzi wanapata mafunzo bora ili ligi na mashindano mbalimbali hapa nchini yapate waamuzi wenye viwango vinavyokubalika.

“Hapa tumeshuhudia kijana mdogo wa darasa la tano David Albert akizawadiwa kuwa mwamuzi bora katika mashindano ya kombe la Meya 2014, lakini bila kuwepo malalamiko juu ya waamuzi, mashindano haya yanayodhaminiwa na Kampuni ya Pepsi (SBC) baada ya kuasisiwa na kuanzishwa na Meya wa Halimashauri Jiji la Mwanza, Stanislaus Mabula hakika naye nimpongeze kwa dhati kwa kulioona hili na kuweza kujitoa kusaidia jamii kupitia michezo,”alisema.

Wito wangu kwa wadau mbalimbali wa michezo kutoa ushirikiano na kuwatumia waamuzi na hata kupeleka vijana wenye vipaji vya soka, waamuzi, riadha na elimu kwa ujumla ili kuwawezesha kupata maarifa zaidi na kuwa matarajio ya Taifa lenye vipaji vya kutosha vyeme kulelewa vyema na msingi mzuri wenye maadili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.