Diwani wa kata ya Levolisi Ephata Nanyaro wakisemezana jambo na Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka katika Uzinduzi wa jiko la shule ya msingi Levolosi iliyoko jijini Arusha lilojengwa na mhisani Daniel Materi kwa gharama ya sh milioni 25 ikiwa ni jitihada ya kuunga mkono mpango wa chakula mashuleni.Picha na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo,Arusha
Shule ya Msingi Levolosi iliyoko jijini Arusha inakabiliwa na ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunza teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ikiwemo kompyuta.
Licha ya serikali kuhamasisha matumizi ya TEHAMA mashuleni ili kusaidia kutunza kumbukumbu ya vitabu vingi na kujifunza kwa njia ya kisasa hata sehemu zenye uhaba wa walimu bado shule nyingi za msingi na zile za kata hazina kompyuta.
Aidha Mkuu wa shule ya msingi levolosi Elisante Kaaya amesema kuwa wamekua wakikosa sehemu maalumu ya wanafunzi kujipatia huduma ya chakula (bwalo) na kueleza kuwa changamotonyingine wanazokutana nazo ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kufundishianakujifunzia Tehama kama kompyuta.
Akisoma taarifa ya shule hiyo katika uzinduzi wa jiko la shule hiyo lilojengwa kwa msaada wa Mfanyabiashara Daniel Materi ikiwani njiamojawapo ya kuunga mkono juhudi za kufanikisha mpango wa chakula mashuleni.
Elisante Kaaya amewapongeza wadau wote waliojitoa kuwezesha watotowa shule hiyo kupata uji kwani mwakani wanatarajia watoto watapata hudumaya chakula cha mchana shuleni hapo.
Mbunge wa Manyara Christopher Ole Sendeka amesema kuwa ni jukumu la jamii kujitoa kusaidia watoto waweze kusoma na kuzingatia taaluma ili waweze kufaulu.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela amesema kuwa ni juhudi nzuri zilizofanywa na ndugu Daniel Materi na kuwataka wafanyabiashara wengine waige mfano wake.
Daniel amesema kuwa msaada huo ni mchango wa kuisaidia jamii inayomzunguka hususani katikamasuala ya elimu ambayo ni muhimu kwa jamii yetu.
|
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.