ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 21, 2014

PINDA KUONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA ML 50 ZA HUDUMA YA AFYA KANDA YA ZIWA.

Afisa Mtenjati wa Taasisi ya Benjamini William Mkapa, Heren Mkondya akizungumza na waandishi wa habari juu ya harambee hiyo.

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, mnamo tarehe 23/08/2014 anatarajia kuongoza harambee ya kukusanya kiasi cha zaidi ya Sh milioni 500 jijini Mwanza, kuchangia Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMAF) inayojishughulisha na uimarishaji wa huduma za afya vijijini nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi Afisa Mtendaji wa BMAF, Heren Mkondya, alisema harambee  hiyo imelenga kukusanya kiasi hicho kutoka kwa wadau, wafanyabiashara, wabunge na viongozi wa serikali na taasisi zake kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga, Kagera na Mara.

Mkondya alisema Mikoa ya Kanda ya Ziwa inakabiriwa na vifo vingi vya akina mama wajawazito ikiwa na wastani wa wajawazito 500 kupoteza maisha kila mwaka, huku asilimia 4 tu ya wajawazito kujifungua katika vituo vya kutolea huduma ya afya, pia takwimu zinaonyesha maambukizi ya Ukimwi yako asilimia 4.8.

“Uhaba wa watumishi wa idara ya afya umeonyesha kuwa asilimia 39 hali inayopelekea kuwepo changamoto kubwa ya utaaji huduma za afya vijijini pamoja na juhudi za serikali kuaji za kutoa ajira bado hali haijakidhi na kupelekea taasisi hii imeajiri watumishi 30 katika Halmashauri sita za awali,” alisema.

Aliongeza kuwa taasisi hiyo imekusudia kuajiri watumishi zaidi ya 150 na kuwapeleka katika Halmashauri zingine zenye mahitaji na kujenga vyumba vya idara ya upasuaji (Theater) 30 ambapo imekusudia kila halmashauri kujengwa mbili katika mikoa ya Kanda ya ziwa,”alisema.

 “Mmoja wa miradi inayotekelezwa na taasisi hii ni “Mkapa Fellows” wa miaka mitano, ambapo sasa unatekelezwa katika Halmashauri 15 katika mikoa ya Shinyanga, Kagera, Simiyu, Rukwa na Zanzibar,”alieleza.

Afisa huyo alisema mbali na mgeni rasmi pia ataambatana na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa ambaye ndiye mwaasisi wa taasisi hiyo na waalikwa wengine

Mtendaji alitoa wito wangu kwa wafanyabiashara wajitokeze kuchangia Mfuko wa mradi wa utoaji wa huduma ya afya vijijini katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kudhibiti vifo vya mama wajawazito kwa wageni mbalimbali watakaohudhulia harambee hiyo itakayofanyika katika Hoteli ya JB Belmont jijini hapa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.