-Shule za sekondari zaidi ya 30 kufaidika na mradi wa vitabu wa Airtel Shule Yetu.
-Airtel kutumia zaidi ya milioni 55 kwa ajili ya vitabu mwaka 2014 -2015
Dar as Salaam, Airtel Tanzania, leo imezindua rasmi mradi wake wenye dhamira ya kuboresha elimu kwa kutangaza shule za sekondari zaidi ya 30 zitakazo faidika na mradi wa vitabu wa Airtel unaojulikana kama Airtel shule yetu.
Akiongea katika mkutano na vyombo vya habari mkurugenzi mkuu wa Airtel, Sunil Colaso alisema “mwaka huu , Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kusaidia elimu kwa kuzipatia vitabu vya sayansi shule za sekondari zaidi ya 30, Tanzania bara na visiwani.”
“Shule zaidi ya 30 zilizochaguliwa ni kutokana na mahitaji makubwa waliyonayo tukisaidiana na Wizara ya Elimu Tanzania. Na huu si mwisho wa zoezi hili, bali mwendelezo wa huduma za kijamii ambazo Airtel inaendelea kuzitoa ikitambua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya elimu Tanzania.”
“Toka tulivyooanza mradi huu wa vitabu miaka kumi iliyopita tumeweza kuzifikia zaidi ya shule 1000 za sekondari zilizopo Tanzania bara na visiwani kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa yote na kuwafikia wanafunzi katika kila kona ya Tanzania.”
“Mwaka huu vitabu tunavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 55 hivyo kila shule iliyochaguliwa watapata vitabu hivi vya sayansi”, alisema Colaso.
Colaso aliongeza kwa kusema “tumefanya kazi kwa pamoja na Mamlaka ya Elimu na Wizara ya Elimu Tanzania kwa kuhakikisha kwamba mahitaji ya vitabu kwa shule zote zilizoingia kwenye mradi huu wa Airtel Shule Yetu kwa mwaka huu tunayatimiza kwa kuwapatia vitabu vya mitaala ya masomo yao kama ilivyo pendekezwa na Wizara”.
“Mwaka jana pia Airtel ilisaidia vitabu vyenye thamani ya zaidi ya milioni 100 tsh kwa shule za sekondari kwa kupitia droo iliyohusisha shule zaidi ya 90” alisema Colaso.
Nae Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa aliongea alisema “Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi tunawashukuru sana Airtel kwa dhamira yenu ya kusaidia jamii kwa kuendelea kuinua kiwango cha elimu hapa nchini ” Airtel kupitia mradi wa Airtel Shule Yetu imekuwa mstari
wa mbele kuiendeleza sekta hii muhimu katika kukwamua watanzania na umasikini”
Mahitaji ya miundombinu na vifaa ikiwa ni pamoja na vitabu hasa vya Sayansi katika shule zetu hapa nchini ni makubwa sana, hivyo shule zitakazopokea vitabu hivi vya mradi wa Airtel Shule yetu, mvitunze na kuvitumia vizuri ili kuunga mkono jitihada za Airtel katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini” aliongeza Mhe. Dkt. Kawambwa.
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Mawasaliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya alisema, “Airtel Tanzania inafurahia kuona maendeleo yanayopatikana katika shule ya msingi ya Kiromo iliyopo Bagamoyo ikiendelea kufaulisha wanafunzi wake baada ya Airtel kuweza kuikarabati shule hiyo na kubadilisha maisha ya walimu na wanafunzi wa shule hiyo.”
“Airtel inatambua umuhimu wa sekta ya elimu na itaendela kutoa mchango ikishirikiana na Wizara na Mamlaka ya Elimu nchini katika ngazi mbali mbali ili kuchochea ukuwaji na mafanikio ya sekta hii.” aliongeza Beatrice.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.