ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, August 24, 2014

SH. BILIONI 1. 1.385,235 ZACHANGWA KUISAIDIA TAASISI YA BENJAMIN WLLIAM MKAPA HIV/AID KATIKA HARAMBEE ILIYOONGOZWA NA WAZIRI MKUU MHE. PINDA JIJINI MWANZA





























MWANZA,
TAASISI ya Benjamini William Mkapa HIV/ADIS Foundation (BWMFA) jana usiku imechangiwa kiasi cha Sh bilioni 1.38 zikiwemo Wizara na Taasisi zake, mikoa sita ya Kanda ya Ziwa,Halmashauri zote, Mashirika, Kampuni, wadau na wafanyabiashara mbalimbali kwenye harambee iliyofanyika katika ukumbi wa JB Belmonte jijini Mwanza.
 
Harambee hiyo iliongozwa na mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Mizengo Pinda, na kuhudhuliwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa (awamu ya tatu), Mawaziri, Manaibu Waziri, Wakuu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ya Mara, Shinyanga, Kagera, Simiyu, Mwanza na Geita, Makatibu Tawala, Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Wenyeviti wa Halmashauri za mikoa hiyo na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara.
 
Awali kabla ya kuanza uchangiaji Rais mstaafu Mkapa ambaye ndiye muasisi wa taasisi ya BWMFA, alisema kwanza haijawahi kutokea, kumekuwa na ushirikiano mzuri wa watumishi wa taasisi hiyo na uongozi wa serikali chini ya Wizara ya Afya, ambapo wamekuwa wakipokelewa na kutekeleza majukumu yao kwa pamoja hali ambayo imeongeza uwajibikaji na kusaidia kuondoa upungufu wa watumishi zaidi katika utoaji huduma za afya kwa wananchi hasa vijijini.
 
“Watumishi wetu walipofika kwenye vituo vya kazi walipokelewa na kusaidiwa hali iliyoonyesha kuwa walikuwa tayari kushirikiana na serikali na siyo kupambana na serikali na hili limejizihirisha leo hapa kutokana na kiongozi mkuu wa shughuli za serikali kukubali kuwa mgeni wetu na mpongeza sana kwa kuendelea kuimalisha uhusiano huo,”alisema.
 
Mkapa alisema katika nchi masikini serikali haziwezi kuwa na uwezo wa kutoa huduma za jamii zote na kuzigharamia, kutakuwa na watu watakaokuwa tayari kujitoa muhanga, kujitoa sadaka lakini siyo kwa kupitia serikali tu ila kwa kushirikiana na serikali.
 
“Nikiwa mwanaCCM kamili nakiri kuwa muumini wa azimio la Arusha, tena niliwahi kuwa Mhariri wa magazeti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali, ambapo azimio hilo lilisema 'ili tuendelee tunahitaji mambo manne, kwanza Ardhi, watu, siasa safi, na uongozi bora', lakini watu wale wanahitaji kujituma na kukusanya nguvu, kwani kidole kimoja hakivunji chawa siyo,”alisema.
 
Aidha aliongeza kuwa, wanapoamua kukusanya nguvu, nguvu yao ile ndiyo inayoweza kusaidia kujiondoa kutoka kwenye umasikini, kwanza wataisaidia serikali lakini pili watakuwa tayari kutoa sadaka kuisaidia taasisi kama ya kwangu ya BWMFA hivyo nawashukuru wote waliochangia tangu ilipoanzishwa na wanaoendelea kutuchangia.
 
“ Kwanza kwasababu wamethibitisha usahihi wa sera hiyo kwamba tukikisanya nguvu tunaweza kupiga hatua kuepuka majanga yanayo tukabili kwenye maeneo yetu,alisisitiza mstaafu huyo na kushangiliwa na waliohudhulia hafla hiyo kwa umakini wake wa kutoa hutuba yenye kusisimua.
 
Naye Waziri Mkuu Pinda, alisema hana shaka na taasisi hiyo kwa kazi iliyokwisha fanya na inayoendelea kufanya kutokana na imani iliyojijengwa ndani ya taasisi hiyo kwani wanachosema ndicho wanachotenda, meweza kufika hapa ni uaminifu wao na ingekuwa tofauti wasingekuwa hapa walipofika leo.
 
“Wamefanya kazi zao katika maeneo ya Nyanda za juu kusini, Zanzibar pia awamu hii imeusisha kwa mara ya kwanza Kanda ya Ziwa ambayo ndio kubwa kuliko Kanda zote ikilinganishwa na Kanda zingine zote nchini kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ambapo takwimu ya sensa ya watu ya mwaka 2000 ilikuwa na watu milioni 6.4 na matokeo ya sensa ya mwaka 2012 iliongezeka mara mbili na kufikia watu wasiopungua milioni 12,”alisema.
 
Pinda alisema ukilinganisha idadi ya watu na uhalisia wa madaktari wanaotakiwa kutoa huduma kwa kanda hii utaona kuwa ni vitu viwili tofauti kwani bado mahitaji ya wahudumu wa sekta ya afya na vituo vya afya ni makubwa sana na changamoto zake bado ni kubwa.
 
“Ukitizama kama nchi utaona daktari moja kuhudumia watanzania elfu ishirini na saba, jeh huyo daktari atakuwa bingwa kiasi gani kufanya shughuli hiyo kwa umakini?, akitolea mfano wa daktari mmoja wa Mkoa wa Mwanza kuhudumia watu elfu 20.4,alisema.
 
Aliongeza kuwa kuwa hiyo tuko hapa kujaribu kuongeza idadi ya madaktari, kujenga miundombinu ya msingi na kupata vifaa katika maeneo mengi ni jambo ambalo taasisi hii imelenga kushirikiana na serikali kuwahudumia wananchi.
 
Katika harambee hiyo iliyogusa Wizara na Taasisi zake, Kampuni nyingi, wafanyabiashara na wadau mbalimbali kuweza kuchangia kiasi cha shilingi bilioni 1.385,235 ikiwa zimevuka lengo lililokusudiwa la kuchangia kiasi cha shilingi milioni 500 kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa na serikali.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.