ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 21, 2014

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUFUTA UMASIKINI KUPITIA UBORESHAJI NISHATI.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema, Serikali imedhamiria  kufuta umasikini kwa wananchi waishio Vijijini kwa kuwapatia nishati ya umeme, hivyo kampuni itakayo suasua kusambaza nishati hiyo kwa kasi inayotakiwa, itanyang’anywa kazi.

Pia ameonya Mameneja wa ‘visingizio’ vya changamoto na kampuni zinazotekeleza miradi hiyo, zitakazoomba rushwa kwa wananchi wanaotaka kufungiwa umeme,ole wao wakibainika.
 Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo jana mjini Biharamulo, wakati akikagua ujenzi wa mradi wa kusambaza umeme katika Vijiji 13 vya wilayani  na Chato mkoani Kagera, unaotekelezwa na kampuni ya kizalendo ya Urban and Rural Engineering Sevrice Ltd. 

Amesema serikali imedhamiria kufuta umasikini na kutoa ajira mpya kwa kuboresha nishati  ya umeme ili kukuza biashara ya wananchi,afya ,elimu na kilimo na ndiyo maana na kuanzishwa kwa mradi wa umeme vijijini.
“Tanzania nzima watu sasa wanafungiwa umeme Vijijini hivyo kila baada ya miezi mitatu tutakuwa tukifanya tathmini ya utekelezaji wa miradi hii, ikifika Oktoba mwaka huu kampuni ambayo haifungi kwa spidi tunaitimua, watu wanataka umeme siyo blablaa.” alisema Waziri huyo.
Alisema ili kufikia malengo na dira ya maendeleo  ya mwaka 2025,lazima tuwe na umeme usiokatikatika ,wa uhakika na wa  bei nafuu, unaopatikana kwa wingi na lazima wananchi wautumie ili kuondokana  na umasikini.
 Aliwaagiza Mameneja wa Tanesco wasimamie kikamilifu ujenzi wa miradi hiyo na kuwaonya waache visingizo vya changamoto na kuwaomba wananchi rushwa.
“Tanesco ya zamani mtu alikuwa anatoa chochote kufungiwa umeme, wananchi wakilalamika katika miradi hii kuwa wanaombwa rushwa, Meneja na mkandarasi ndiyo mtakaoumia. Ole wenu wananchi waombwe rushwa, naomba tanesco ya sasa ifuate maelekezo na maadili wananchi wapate umeme kwa sh 27,000 bila rushwa.” alieleza.
Akilelezea hatua za Wizara yake kuondoa kero ya kukatika katika kwa umeme, Profesa Muhongo i alisema  serikali imeagiza mitambo miwili mipya ya kufua umeme wa kutumia mafuta kutoka nchini Uholanzi itakayo kuwa na  uwezo wa kuzalisha Megawati 2.50 (kila mmoja megawati 1.25), na itafungwa Biharamulo.
“Mtambo huu wa sasa uliopo katika kituo cha kuzalisha umeme hapa, umechakaa. Unatumia gharama kubwa ya sh milioni 300 kwa mwezi lakini hatuna namna kwa sababu wananchi wanataka umeme na sisi tumpania kuondoa umaskini kwa kuwapa wananchi husuasan wa vijijini umeme, tunawaletea mitambo miwili ya kufua umeme Biharamulo na Chato.” alieleza.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akitoka kukagua shughuli zinazoendelea katika kituo cha kuzalisha umeme cha kampuni ya Tanesco kilichopo wilayani Biharamulo.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Katoke wilayani humo akiwemo Fravian Daniel walimwambia Waziri huyo wakati akikagua ujenzi wa mradi wa kutoka Katoke kwenda Runazi (km 23) kuwa mara kwa mara umeme wa wilaya hiyo umekuwa ukikatika katika hovyo, hivyo wanaomba tatizo hilo liondolewe.

Meneja wa Tanesco wilayani Biharamulo Mhandisi Ernest Milyango, alimueleza Waziri Muhongo kuwa rushwa haipo katika utekelezaji wa miradi hiyo na kudai kuwa ifikapo Oktoba mwaka huu wataanza kutoa fomu za maombi ya wateja kuunganishiwa umeme kwa njia ya electroniki.
Alisema utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika vijiji 13 vikiwemo vitatu vya wilaya ya Chato unaenda vizuri na wanatarajia utakamilika ifikapo Januari 2015.
Awali Mratibu wa mradi  Mhandisi Julius Kateti wa kampuni ya Urban and Rural Engineering Ltd , alisema kampuni yake inajenga vituo vinne vya njia ya msongo mkubwa wa umeme (HT Line) kutoka Katoke Mission –Nyakahura, Busala-Ilemela, Katoke- Lunazi na Superline-Kasenga.
Majadiliano kati ya wananchi na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo yakiendelea.
Huu ni usimikaji wa nguzo kwaajili ya usambazaji umeme ndani ya vijiji vya wilaya ya Biharamulo na wilaya jirani, na hapa mafundi wakiendelea na kazi.
Waziri Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akipata maelezo toka kwa Injinia Charles Arch anayesimamia usimikaji wa nguzo kwaajili ya usambazaji umeme vijijini na hapa akiwa katika ujenzi wa njia ya umeme kutoka kijiji cha Katoke kuelekea Lunazi umbali wa Kilimeta 23.
Usimikaji wa nguzo kwaajili ya usambazaji umeme vijijini katika ujenzi wa njia ya umeme kutoka kijiji cha Katoke kuelekea Lunazi umbali wa Kilimeta 23, ukiendelea.
Waziri Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akitoa ufafanuzi juu ya harakati za Serikali kufikia malengo ya Millenium kupitia suala la uboreshaji wa upatikanaji wa nishati vijijini. KUMSIKILIZA BOFYA PLAY.
Waziri Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza  na wanafunzi wa shule ya Seminari ya Katoke Jimbo la Rulenge Ngara mkoani Kagera, ambapo aliwahimiza kuchangamkia masomo ya Sayansi kwa taifa bado linahitaji mafundi na wataalamu wa fani mbilimbali.
Waziri Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza  na wanafunzi wa shule ya Seminari ya Katoke Jimbo la Rulenge Ngara mkoani Kagera, ambapo aliwahimiza kuchangamkia masomo ya Sayansi kwa taifa bado linahitaji mafundi na wataalamu wa fani mbilimbali.
Wanafunzi wa shule ya Seminari ya Katoke Jimbo la Rulenge Ngara mkoani Kagera na umakini wao.
Waziri Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza  na wanafunzi wa shule ya Seminari ya Katoke Jimbo la Rulenge Ngara mkoani Kagera, ambapo aliwahimiza kuchangamkia masomo ya Sayansi kwa taifa bado linahitaji mafundi na wataalamu wa fani mbilimbali.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.