ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 5, 2014

NDANI YA USIKU MMOJA FLORA SALOON AWATAMBULISHA MISS LAKE ZONE NA MISS MWANZA

Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akiwasha mshumaa wa rangi ya pinki kuashiria kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake, katikati akishuhudiwa na Mwandaaji wa Miss Lake Zone 2014 Flora Saloon na kulia kabisa ni Mc wa usiku huo wa kutambulisha tu wanyange wa vinyang'anyiro vya Miss Mwanza na Miss Lake Zone.
Mwandaaji wa Miss Lake Zone 2014 Flora Saloon akitoa maelezo juu ya mchakato na tarehe rasmi ya Redds Miss Lake Zone 2014 ambayo itafanyika tarehe 30/08/2014.
Huku akiitaja na historia kumlinda Muandaaji wa Redds Miss Mara Brother ameahidi kuleta changamoto kwenye kinyang'anyiro cha Miss Lake Zone.
Sehemu ya wanyange 12 wa Redds Miss Mwanza ambao mwishoni mwa wiki hii watashuka katika ukumbi wa JB Belmonte kuonyeshana skillz hatimaye mmoja kuibuka kinara.
Kama ni burudani huyu hapa Mzee Yusufu.
Mzee Yusufu na mashabiki wake wa Mwanza.
Kutoka kulia ni Brother David Lata, mwandaaji wa Redds Miss Mwanza John Dotto (katikati) na mdau wa kamati. 
Ng'aring'ari ...
Meza ya wastaarabu.
Ni tukio lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi mpya wa kisasa wa Mamiz uliopo Mkolani jijini Mwanza.
Kalla Jeremiah (kulia) akiwa na mdau wa Kamati ya maandalizi ya Redds Miss Lake Zone 2014.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.