ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 20, 2014

HII LEO MWANZA HAKUNA BIASHARA WAFANYABIASHARA WAGOMA KUFUNGUA MADUKA.

MKURUGENZI wa Jiji la Mwanza Halifa Hassan Hida ameeleza kukutana kesho na viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiasha (JWT) ili kusikiliza hoja za madai yao yaliyopelekea kuhamasisha mgomo wa wafanyabiashara wa maduka leo jiji hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Hida amesema kwamba hatua ya JWT kuhamasisha mgomo ulioanza jana kwa madai ya kutosikilizwa na uongozi wa jiji si kweli na mgomo huo ni batili haukubaliki.

“Nimekutana nao zaidi ya mara tano nikiwataka wawasilishe madai yao kwa maandishi ili kuyatafutia ufumbuzi lakini wamekuwa wakishindwa kufanya hivyo pamoja kukutana na kuwasiliana nao zaidi ya mara tano, naaona sasa wamehamasisha mgomo kwa wafanyabiashara wengine kitu ambacho si cha kiungwana na madai kuwa nimekataa kukutana nao si kweli ,”alisema.

Hida amefafanua kuwa pamoja na kuwataka viongozi hao kuwasilisha madai yao kwa maandishi tangu tarehe 31 mwezi Mei mwaka huu lakini wameshindwa kufanya hivyo hata pale walipotakiwa kukutana naye ili kuyatafutia ufumbuzi bado hawakuwa tayari.

“Hakuna jambo ambalo halizungumziki, tuliwataka wawasilishe madai yao hawakufanya hivyo pamoja na kukutana nao kwenye kikao na Mkuu wa Mkoa Mhandisi Evarist Ndikilo na kuelezwa walete madai yao kwa maandishi lakini pia wamekuwa wakiwasiliana na mimi zaidi ya mara tano nikiwasisitiza hilo bado hawakuwa tayari illi kuwezesha tukae na kitafutia ufumbuzi wa madai yao,” alisisitiza.

Mkurugenzi Hida amesema kuwa,  sasa wamekubali kukutana na uongozi wa jiji na kuwasilisha madai yao kwa maandishi, atakaa na viongozi na wawakilishi wa JWT kesho kwenye kikao cha pamoja katika ukumbi wa halmashauri ya jiji hilo na kutolea ufafanuzi wa madai yao.

Wito wangu kwa wananchi na wafanyabiashara wa jiji la Mwanza kuwa watulivu na waendelee na shughuli zao za kila siku ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara kufungua maduka ili kutoa huduma kwa wananchi wakati uongozi wa jiji na JWT wakitafutia ufumbuzi wa madai yao kwa kukaa mezani kwa mazungumzo na kutoa ufafanuzi na maafikiano.
Moja kati ya vipeperushi vya mgomo vilivyokuwa vikisambazwa kwa wafanyabiashara wote jijini Mwanza kuhamasisha mgomo. 
JWT WANASEMAJE!
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara (JWT) Christopher Wambura alisema kwamba wameamua kuanza mgomo huu kutokana na uongozi wa Jiji kutosikiliza madai yetu kwa muda mrefu na kupelekea kukithiri kwa kero mbalimbali bila kupata ufumbuzi wake.

Wambura amesema kuwa kutokana na Mkurugenzi Hida kutokutana na JWT ili kushughulikia madai yetu kumeonekana kutupuuza na njia pekee tuliyoamua kuchukua ni kuhamasisha mgomo wa wafanyabiashara wote hadi hapo madai yetu yatakaposikilizwa na kutatuliwa na uongozi wa jiji.

Mwenyekiti huyo alitaja baadhi ya madai ya wafanyabiashara  kuwa ni pamoja na kukamatwa kwa mikokoteni inayotumika kubeba bidhaa za wafanyabiashara kutoka kwenye maghara kuleta dukani, tozo za leseni za Halmashauri ya kuwa na gharama kubwa hali inayosababisha wafanyabiashara wengi kutomudu, tozo za usafi wa taka kwa kila mwenzi kwa kila duka kuwa juu.

Madai mengine ni Halmashauri ya Jiji kushindwa kuwaondoa Wamachinga wanaofanya biashara na kupanga bidhaa hadi kwenye milango ya maduka yao, kukamatiwa bidhaa zao na magari yanapokuwa yanashusha kwenye maduka mjini na Mgambo wa jiji kuchukua bidhaa bila kufuata utaratibu hali inayopelekea kupoteza mali zao.

“Tukutane na Mkurugenzi kuzungumzia madai yetu ili kuyatafutia ufumbuzi wake, endapo ataendelea kukataa kukutana naye basi wafanyabiashara wamedai kuendelea na mgomo hadi hapo watakaposikilizwa kero za madai yao,”alisisitiza.

Aidha Wambura amesema katika mgomo huo wa amani hautasitishwa na kulazimisha wafanyabiashara wengine bali wafanyabiashara wameamua kuungana kwa hili ili kuhakikisha madai ya kero mbalimbali tuliyokwisha wasilisha kwa uongozi wa jiji yanatafutiwa ufumbuzi wa haraka ili kumaliza hali hii iliyoanza kutekelezwa.


Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiasha wa Viwanda na Kilimo (TCCIA), Elbariki Mmari akizungumza na waandishi jana alisema kwamba mgomo huo ni batri kwa kuwa wafanyabiasha wa jiji la Mwanza si wanachama wa Jumuiya hiyo.

“Hoja na madai yao tumesikia lakini hazina msingi wa kuhamasisha mgomo na haya madai yao mengi yameishwa fanyiwa kazi na Halmashauri ya jiji tangu mgomo wa kwanza ambao uongozi wa Serikali ya Mkoa, Halimashauli yaa Jiji, TRA, TCCIA na JWT tulikaa na Mkuu wa mkoa tulizungumza na kufanyiwa kazi ikiwa zingine TCCIA kushinikiza kutekelezwa,”alisema.

Mmari alisema kwamba baadhi ya hoja ambazo jiji imezifanyia kazi kupitia kikao cha pamoja zilizoazimiwa ni Jiji kuwaondosha wafanyabiashara wadogo “Machinga” kufanya shughuli zao na kupanga bidhaa hadi kwenye milango ya maduka ya wafanyabiashara wengine, kuondolewa kwa mikokoteni kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria za Mipango Miji zilizopitishwa.

“Na hili hata ukitembea Miji na Majiji makubwa nje hakuna mambo ya matolori, mikokoteni na badala yake sasa wanatumia Bajaji na gari ndogo kufanya kazi hizo hivyo hoja hii haina mashiko, tayari Jiji limewaondoa Machinga kila mtu ni shahidi , Halmashauri ilipiga marufuku lipo kisheria wafanyabiasha kuacha kupanga bidha nje ya maduka kwa kuwa wanazuia njia za watembea kwa mguu,” alisema .

Aidha suala la leseni kweli ziko juu lakini Mkurugenzi mengine hana mamlaka nayo yanatoka Wizarani, juu ya tozo za uchafu hili linazungumzika lakini siyo kuhamasisha mgomo, lakini wafanyabiasha ni wanachama wa TCCIA hivyo wanapofungua maduka yao wanabuguziwa kwa vitisho kuwa watapigwa na kuharibiwa mali zao hili tunalipinga kwa nguvu zote , hivyo ni vyema wakachwa waendelee na kufungua maduka.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.