NA PETER FABIAN, SENGEREMA.
TIMU za vijiji zaidi ya 110 vya Kata za Jimbo la
Sengerema kumwagiwa mipira kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kucheza mashindano
ya kupata wachezaji watakaunda timu za Kata za jimbo hilo katika mashindano ya
Kombe linaloandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mbunge wa Jimbo la
Sengerema William Ngeleja kwa nyakati tofauti kwa wananchi kwenye mikutano ya
hadhara katika Kata za Busisi,Nyamatongo, Nyampande, Ngoma wakati wa ziara yake ya
kikazi inayoendelea ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza hoja za wananchi jimboni humo kupitia utaratibu uliozoeleka.
Ngeleja aliwataka vijana katika maeneo mbalimbali ya
vijiji vya Kata za Wilayani humo kuanza kupasha misuri kabla ya timu za Kata
zote kuanza kushiriki mashindano ya kombe analoliandaa ambapo aliwaeleza vijana
kuwapatia vifaa ikiwa ni mipira kwa timu za vijiji na timu za Kata zote
kuzipatia kila moja jezi seti moja na mipira miwili zitakazoshiriki mashindano
hayo.
“Tukimaliza mambo ya Brazil na kombe la dunia
tunaanza na sisi kupasha misuri yetu kujiweka sawa na mashindano makubwa ya
jimbo letu ya kombe la Mbunge hivyo kaeni mkao wa kujiweka fiti kwa mazoezi, baada
ya mfungo wa ramadhani kazi inaanza mara moja,” Alisema.
Mbunge Ngereja alisema kwamba mashindano ya mwaka
huu yatakuwa na utofauti kidogo baada ya kuboreshwa ambapo vifaa
vitakavyotolewa ni vyakiwango cha kwa mipira na jezi huku zawadi za mshindi wa
kwanza hadi watatu zikiongezeka pamoja na kipa bora, mfungaji bora,na timu
iliyoonyesha nidhamu katika mashindano hayo ya mwaka huu 2014.
Ngeleja pia alitoa wito kwa viongozi wa Vijiji, Kata
na timu kuanza mikakati ya maandalizi ya timu zao huku akiwataka kuwapuuza
baadhi ya wapinzani wake kisiasa wanaopita kumchafua kwa madai kuwa mwaka huu
mashindano hayo hayatakuwepo kutokana na kushindwa kuwaletea vifaa, “waelezeni
yapo na wataona wenyewe wakati tutakapoanza kugawa vifaa hivyo,” alisisitiza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.