ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 15, 2014

MARA BAADA YA 'KEKUNDU' AIC MAKONGORO VIJANA KWAYA SASA KUJA NA 'KEUSI'

Stahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akitoa maelekezo kwa mafundi wa ujenzi wa jukwaa litakalo tumika kwenye uzinduzi wa album ya 'Keusi' toka kwao Aic Makongoro Vijana Kwaya  ambao wanategemea kuzindua hivi karibuni katika viwanja vya kanisa la Aic Makongoro jijini Mwanza.  Album hiyo inakuja ikiwa sasa ni takribani miaka mitano sasa imepita tangu kwaya hiyo ilipozindua album yake ya kwanza iliyowatambulisha vyema kwenye soko lamuziki wa injili iliyojulikana kama 'Kekundu'.
Mfundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa jukwaa ambalolitakuwana ukubwa wa kuweza kumiliki idadi kubwa ya wanamuziki na vyombo vyao either wa bendi au kwaya za kuimba na kumtukuza Mungu.
Mhe. Mabula akitia msisitizo ili shughuli hiyo imalizike kwa ufanisi. 
Mbali ya kufanya kazi hii kama sehemu yake ya majukumu ya kuitumikia jamii anayoiongoza na kuhakikisha ustawi wake, vilevile Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza amefanya ukaguzi huu akiwa ni mmoja wa wana kamati wa Kamati ya Uzinduzi wa Album hiyo (Keusi) inayosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa muziki wa Injili kanda ya Ziwa,
Wakiwa na kiu ya kujua kwanza kwanini iitwe Keusi,
Nini kimeimbwa ndani yake,
Kimelenga nini na ni simulizi juu ya nini....??

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.