Wananchi wakisikiliza kwa umakini uwasilishaji Kero kwenye mkutano wa mbunge wa Jimbo la Sengerema William Ngeleja katika kijiji cha Busisi jana. |
Sehemu ya mkutano. |
Wazee wa mji. |
Viongozi na Baraza la wazee. |
Wananchi wakisikiliza kwa umakini uwasilishaji Kero kwenye mkutano wa mbunge wa Jimbo la Sengerema William Ngeleja katika kijiji cha Busisi jana. |
Viongozi meza kuu waliokuwa kwenye ziara ya mbunge ya kukagua miradi ya Maendeleo jimboni humo katika kata za Busisi, Nyamatondo na nyingine jimboni humo. |
Robert Mathayo akitoa Kero ya uhaba wa maji, ardhi na zahanati kwenye mkutano wa mbunge wa Jimbo la Sengerema William Ngeleja katika kijiji cha Busisi jana. |
MBUNGE wa Jimbo la Sengerema William Ngeleja amecharukia baadhi ya watendaji wa Halmashauri Wilaya hiyo wanaokwamisha utekelezaji wa Ilani na wanaochakachua fedha za miradi ya maendeleo.
Ngeleja alitoa kauli hiyo juzi wakati akihutubia wananchi wa kijiji cha Busisi Kata ya Busisi wilayani humo wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri na kusikiliza hoja za wananchi katika maeneo mbalimbali ya Kata za jimbo hilo.
Mbunge huyo alisema kwamba Halmashauri hiyo itaendelea kuwawajibisha watumishi na watendaji wanaokwamisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010/2015 na wanaochakachua fedha kwa kutumia nafasi zao za kiutendaji na kusababisha kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hata kutokamilika kwa wakati na chini ya kiwango.
“Tutaendelea kuwachukulia hatua za kimaadili ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha watumishi na watendaji wabadhilifu wa fedha za miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri yetu ambao wanasababisha wananchi kuilalamikia Serikali ya Chama Cha Mapinduzi iliyopo madarakani kwa kukosa huduma muhimu kwenye maeneo yao,”alisema.
Akizungumzia watumishi hao alisema kwamba hadi sasa Halmashauri hiyo kupitia Baraza la Madiwani kwa kushirikiana na viongozi wa serikali na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya imewawabisha tatumishi wapatao 13 waliothibitika kutenda ubadhilifu wa mamilioni ya fedha za miradi ya maendeleo.
“Hapa Busisi tulizindua mradi wa maji toka ziwa Victoria tangu mwaka jana mwezi wa Februari lakini leo Pampu iliyokuwa inasukuma maji kwenda kwenye tanki iliondolewa na watendaji wa maji na kuletwa Pampu mbovu ambayo karibu mwaka hakuna hata kinachoendelea na kusababisha wananchi kupata usumbufu wa maji wakati wako jirani na ziwa na majibu hayatulidhishi,”alisisitiza.
Hatua hiyo inafuatia majibu ya Mhandisi wa Idara ya Maji wa halmashauri hiyo Barnabas Kishina kushindwa kutoa majibu sahihi, wakati alipotakiwa na Mbunge Ngeleja kujibu kwa wananchi waliouliza swali la kero ya kutopatikana maji wakati Pampu yake mpya ilitolewa na kuletwa mbovu ya zamani jambo ambalo liliwafanya wananchi kulalamika na kudai kupata adha ya upatikanaji wa maji safi.
Ngeleja aliwabeza wapinzani wake wa kisiasa jimboni humo wanaopita kumchafuwa na kumtolea lugha ya kejeli na matusi kwa hajafanya kitu huku yeye akitaja kutekeleza miradi ya umeme katika kila kijiji jimboni humo, maji na sasa anaendelea kumalizia baadhi ya miradi ya Afya, Elimu na Miundombinu ya barabara baada ya Halmashauri kununua Greda kufanya kazi hiyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.