ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 11, 2014

KUKU NILIYEMFUMA SENGEREMA...!!

Ni kuku asiyekuwa na manyoya amefumwa na kamera ya mtandao huu katika kijiji cha Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Manyoya au magoya kama wengine wanavyoyaita humsitiri kuku katika mvua, kujikinga na baridi kwa kumpa joto, hutumika kama kinga ya kuchomwa na vitu vyenye ncha kali kwani ngozi ya ndege ni laini, hivyo anapoingia kwenye purukushani hususani vichaka vyenye miiba hawezi kudhulika. Sasa anapokuwa katika hali hii ya kukosa magoya ni shida.
Ndege huyu yuko tayari tayari, ni kisu chako tu, haitaji kunyonyolewa!! Cha ajabu si mwewe wala ndege mwarabu (sijui ndiyo ndege aina ya Tai) wala wanyama wakali kama mbwa wote hawajawahi kumdhuru kuku huyu zaidi ya kumpita tu. Duh  na uroho wote walionao ..Maajabu..!

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.