Airtel yamwagia wahariri vifaa vya michezo
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetoa msaada wa vifaa vya michezo wenye thamani ya Sh milioni 1.1 kwa timu ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema uamuzi wa kutoa msaada huo umefikiwa kutokana na kutambua mchango wa vyombo vya Habari nchini.
“Tunafaurahi kuwaambia kwamba leo (jana),tunakabidhi msaada wa vifaa vya michezo ndugu zetu wahariri ambao wanajiandaa na mchezo wa kirafiki mkoani Mtwara Jumamosi hii.
“Kama kwa vile wahariri ni watu ambao wanakuwa na majukumu mengi ya kila siku kwenye vyumba vya Habari, tunaamini baada ya mkutano wao, watapata fursa ya kucheza mchezo wa soka pale Mtwara ili kuweka miili yao sawa,”alisema Mmbando.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni pamoja na jezi seti moja, mipira mitano, filimbi tatu, fulana na traksuti tano.
“Hii ni sehemu tu ya msaada mdogo,tunategemea vitawasaidia jamaa zetu kuonyesha makekeo yao,”alisema Mmbando.
Akipokea msaada huo, Nahodha wa timu ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Kulwa Karedia aliishukuru Airtel kwa msaada huo na kusema umekuja wakati mzuri.
“Unajua mawasiliano bila waandishi wa habari hayapo, nadhani ndiyo maana Airtel wameona umuhimu wa kutoa msaada huu na sisi tunasema hatutawaangusha,”alisema Karedia.
Alisema timu yake inatarajia kuondoka kesho kuelekea Mtwara ambako Jumamosi hii watacheza na timu ya waandishi wa habari mkoa wa Mtwara.
Kikosi cha TEF kinaundwa na wachezaji kama Theopil Makunga,Revocatus Makaranga, Jesse Kwayu, Manyerere Jackton, Ansbert Ngurumo, Salehe Mohamed, Neville Meena, Mnaku Mbani, Salim Said Salim, Wallace Maugo na Erick Anthony ‘Chinga’.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.