ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 9, 2014

CCM KIRUMBA YAJIZATITI KUHAKIKISHA BAADHI YA MICHEZO YA KIMATAIFA INAFANYIKA MWANZA.

Vyumba vya kubadililishia nguo wachezaji viko katika ukarabati uwanjawa CCM Kirumba jijini Mwanza, ikiwemo maboresho ya mfumo wa maji safi na maji taka.
Upakaji rangi kuta za vyumba hivyo unaendelea ndani, sanjari na uwekaji sakafu maridhawa na kuboresha mifumo ya umeme.
Zana zote zilizochoka hazihitajiki kwenye vyumba vya mapumziko kwa wachezaji na waamuzi ndani ya uwanjawa CCM Kirumba Mwanza.
Dimbani.
NA ALBERT G. SENGO; MWANZA
Mara baada ya mkoa wa Mwanza kukosa michezo kadhaa ya Kimataifa ikiwemo mashindano ya kufuzu kwenda CHAN, kutokana na uwanja wake wa CCM Kirumba kukosa sifa za kukidhi matakwa ya FIFA,  hatimaye wamiliki wa uwanja huo Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza wameanza ukarabati kwa kuzifanyia kazi kasoro zote zilizo bainishwa na Kamati  ya Ufundi ya TFF iliyodhuru mwaka jana mkoani humo kuukagua uwanja huo kuona kama una kidhi viwango vya Kimataifa ili baadhi ya michezo ipate kuchezwa mkoani humo hatua ambayo ilishindikana kwa uwanja huo kukosa sifa.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) Nasibu Mabrouk amezitaja changamoto ambazo zimeanza kufanyiwa kazi ni pamoja na kuwa na vyoo na bafu visivyopungua vinne katika kila chumba cha wachezaji, Mfumo wa maji safi kuwa madhubuti na maji yaweze kutoka kwenye mabomba na kutumika vyooni badala ya style ya sasa ya kutumia ndoo na makopo, Vyumba vya wachezaji na waamuzi kupakwa rangi na kuwa na mwonekano wenye hadhi, Umeme uunganishwe ili taa ziweze kuwaka kwenye vyumba vya wachezaji na waamuzi.

Aidha Mabrouk amesema kuwa ukarabati pia utahusu benchi za wachezaji wa akiba kwa kuongezwa ukubwa kwani idadi ya wachezaji na viongozi imeongezeka na benchi zilizopo sasa hazikidhi mahitaji kiasi cha kufanya wachezaji wengine kukaa chini.

Matangazo ya biashara yaliyoko kwenye kuta za uwanja hayatakiwi kuonekana wakati wa mchezo endapo siyo wadhamini rasmi wa mchezo husika.

Zaidi BOFYA PLAY KUMSIKILIZA 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.