ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 11, 2014

AIRTEL NA MOJIFA WAANZA USHIRIKA WA KUTUNZA MAZINGIRA MIKOANI... WAANZIA ARUSHA.

Mkuu wa shule ya sekondari Sing’isi mwalimu Upendo Kanana akipanda mti katika viwanja vya shule ya sekondari Sing’isi wakati wa siku maalumu ya upandaji miti zoezi lililoendeshwa na wafanyakazi wa kampuni ya AIRTEL Arusha  huku wanafunzi wa shule hiyo nao wakishiriki tendo hilo jana
Na Mwandishi wetu.
Kampuni ya simu za mkononi Airtel kwa kushirikiana taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na shughulu za utunzaji wa mazingira ‘Sustainable Enviromental’ ya Moivaro Jitegemee Family (MOJIFA) leo wamefanya shughuli ya upandaji miti kwa shule za sekondari mkoani Arusha katika kijiji cha Sing’isi wilayani Arumeru mkoani Arusha

Airtel na taasisi hiyo binafsi na  wadau mbalimbali katika utunzaji wa mazingira wamechukua hatua stahiki za kuhifadhi mazingira ili  kupunguza wimbi la uharibifu wa vyanzo  vya maji katika  maeneo mbalimbali nchini.

tukio hilo maalumu la upandaji wa miti  lililoongozwa na  wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mkoa wa Arusha, katika shule ya sekondari  Sing’isi.

Meneja biashara na mauzo kanda ya kaskazini Brighton Majwala alisema “airtel imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya elimu nchini na safari hii tumeamua kupanda miti hii ili  kuwahamasisha wanafunzi kutambua umuhimu wa kutunza mazingira  ambayo yana mchango wa moja kwa moja katika kujifunza kwao”
Nae  mkuu wa shule ya sekondari Sing’isi  upendo Kakana ameishukuru kampuni ya airtel kwa kuendesha zoezi hilo  katika shule hiyo na kuongeza kuwa kijografia shule hiyo ipo katika eneo lenye upepo mkali wa mara kwa mara na kwa maana hiyo kuwepo kwa miti ya kutosha  katika eneo la shule kutasaidia kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na upepo.

DIWANI wa Sing’isi mh, Peter kiyungai alitoa rai kwa wananchi wote kuendelea na zoezi la kupanda miti kama walivyofaya Airtel na kutunza mazingira hasa maeneo ambayo ni vyanzo vya maji kwani kwa kutofanya hivyo ni dhahiri tunahatarisha maisha yetu wenyewe kwa kuwa hatar ya kukosekana kwa maji hayo kutokana na uharibifu wa mazingira huenda ikapelekea hata kupotea kwa Amani ya maeneo husika 
Mgeni Rasmi wa tukio hilo maalum Bi Recho Ngowi ambae ni Afisa mtendaji wa kata ya Sing’isi aliipongeza Airtel na taasisi hiyo binafsi ya MOJIFA pamoja na  wadau mbalimbali wa maendeleo  waliohudhuria katika upandaji miti na utunzaji wa mazingira katika kijiji cha Singisi

“Naahidi kuwa jitihada hizi zitaendelezwa na serikali ili kuhakikisha nchi haiingii katika changamoto ya kukosa uhai kwa janga la uharibifu wa mazingira yetu” alisema Bi Recho

Kampuni ya simu za mkononi tawi la Arusha kwa kushirikiana na taasisi ya MOJIFA wamepanda jumla ya miti 200 na kuahidi  zoezi hilo kuwa endelevu katika maeneo mengine yenye uhitaji wa miti.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.