Na PETER FABIAN,
MWANZA.
MEYA wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (CCM) amewataka wahitimu wa vyuo vikuu nchini wasiwe na mtizamo pekee wa kuajiriwa bali wawe na dhana ya ujasiriamali.
Mabula ambaye ni Diwani wa Kata ya Mkolani, aliyasema hayo jana akiwa mgeni rasmi kwenye mahafari ya kuwaaga vijana wa Umoja wa Kikiristo Wanafunzi Tanzania(UKWATA) wahitmu katika Chuo cha Mipango Mwanza .
“ hivi sasa matarajio makubwa ya vijana mnaohitmu katika vyuo vikuu mbalimbali nchini ni mnamtamo wa kuajiriwa na serikali lakini bado mnaowajibu wa kujifunza bila kuwazia ajira pekee za serikali na kufikiria zaidi fursa za ujasiriamali,” alisema.
Pia kuna baadhi ya wahitimu wamekuwa na mwelekeo wa kuingia katika ulingo wa siasa lakini ulimwengu wa kisasa kataika siasa ni tofauti na siku za nyuma hivyo wasomi mnapaswa kuwasaidia wenzenu wasio waelewa ili kuendea kuhubiri amani na upendo kujenga umoja wa utaifa wetu.
“ ni kweli taifa lina bomu ambalo ni ukosefu wa ajira kwa vijana hivyo ni vyema vijana mkajitambua na kutumia elimu yenu kuhakikisha mnasimamia na kuilinda misingi imara iliyoaachwa na waasisi wa taifa hili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali kufikia malengo tuliyojiwekea,” alibainisha.
Awali wahitimu UKWATA wakisoma risala kwa mgeni rasmi Imani Magawa na Rahel Sendeu waliomba kusaidiwa vifaa vya muziki wa injili, vitambaa kwa ajili ya madhabahu ambavyo gharama yake ni kiasi cha milioni 5.2 ili kuwezesha kwaya ya UKWATA na Vijana Bwiru AICT kukamilisha tungo za nyimbo.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Tumaini cha jijini Dar es salaam Godwin Gondwe ambaye alipata fursa ya kuwaasa vijana hao kutojiingiza katika siasa zenye mwelekeo wa kuwagawa watanzania na kulisambaratisha taifa badala yake wazingatie taaluma walizopata ili kuwajengea uwezo wa kuajiriwa mahala popote pia kujiajiri katika ujasiriamali.
Gondwe, maarufu kwa jina la dabo “G” ambaye pia ni mtangazaji wa kituo kimoja cha Luninga nchini alikubali kuchangia gharama zitakazohitajika kwa vitambaa vya mapambo na madhabahu ambapo fedha zake atazitoa baada ya kuwasilishwa gharama zake.
Huku Meya Mabula akichangia kiasi cha Shilingi milioni moja mbali ya kuwalisha keki wahitimu wote wa UKWATA kwa shilingi laki nne pia zikachangwa jumla ya shilingi laki sita nyingine kutoka kwa wahitimu na waalikwa.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.