ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 4, 2014

KIGOMA WACHANGISHA ZAIDI YA MILIONI 263.8 KUTEKELEZA MRADI WA UJENZI WA SEKONDARI YA SAYANSI


 NA PETER FABIAN, MWANZA.

MKOA wa Kigoma umekusanya kiasi cha Sh. milioni 263.8 kwa ajili ya kutekeleza mkakati wake mkubwa wa ujenzi wa sekondari ya mchepuo wa sayansi kidato cha tano na sita (Kigoma Science Grand High School) katika uchangia wa wananchi na watu wanaotoka mkoani humo.

Hatua hiyo imelenga kutekeleza ujenzi huo kutokana na changamoto inaoukabili mkoa huo wa kuwa na sekondari moja ya Malagarasi yenye mchepuo wa sayansi hali ambayo imekuwa ikiwanyima nafasi vijana wengi wa masomo ya sayansi kupata nafasi ya kuendelea na masomo mkoani humo na kulazimika kwenda mikoa ya jirani jambo ambalo baadhi huwakatisha tamaa.

Akizungumza juzi kwenye hafla ya harambee fupi ya uchangiaji wa ujenzi huo jijini Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya alisema kwamba, tangu kuanzishwa kwa mkakati huo tayari mkoa huo umeishafanya harambee sehemu tofauti ikiwa ni jijini Dar es salaam, Kigoma na Mwanza.

Mchibya alisema kwamba kiasi cha fedha kinachohitajika katika mradi wa ujenzi huo ni bilioni 28 ikiwa ni ujenzi wa madarasa, majengo ya ofisi za utawala, maabara tatu, mabweni na bwalo la chakula na mikutano, Samani za ofisi, jiko, matundu ya vyoo na viawanja vya michezo, hivyo ni mradi ambao unaitaji michango mbalimbali ya fedha na vifaa kwa wadau wa mkoa huo na wanaotoa mkoani humo.


“Leo tuko jijini mwanza kuhamasisha wananchi wanaotoka mkoa wa Kigoma , marafiki, wafanyabiashara na wadau mbalimbali lengo ni kuchangia na kukusanya kiasi kikubwa cha fedha kitakachowezesha kuanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi huo ili kuweka mazingira bora ya kujifunzia wanafunzi,”alisema.
Luteni Kanali msataafu Machibya alisema kwamba, wadau wa elimu na wananchi waishio nje ya Mkoa wa Kigoma ni vyema wakaitikia wito wa maboresho ya elimu kwenye Nyanja zote ikiwa ni kuanzia elimu ya msingi, sekondari, vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Juu.

“Mkoa unazo shule za msingi 635 zikiwemo za serikali 627 na binafsi 8, sekondari 168 za serikali zikiwa 126 na sekondari binafsi 42, Vyuo vya Ualimu vine kati ya hivyo vya serikali ni viwili, binafsi kimoja na dini kimoja ambapo vyuo hivyo vinatoa wahitimu ngazi ya Cheti kwa walimu wa shule za msingi na Stashahada kwa walimu wa Sekondari,”alisema.
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Uchangishaji ya Mkoa huo Erasto Sibora alisema kwamba kutoa ni moyo hivyo kila mwananchi na marafiki wa mkoa wa Kigoma wanao wajibu wa kuchangia mapinduzi makubwa ya uboreshaji wa Elimu mkoani humo ikiwemo ujenzi huo wa sekondari ya maoso ya sayansi.

Akitangaza kiasi cha fedha kilichochangwa na kupatikana katika harambee hiyo Sibora alisema kwamba jumla ya Sh milioni 10.8 zimepatikana ikiwa tasilimu milioni tano na tano zingine ni ahadi kutoka kwa waliohudhulia lakini pia akifafanua kuwa uchangiaji huo endelevu hadi watakapokamilisha ujenzi huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.