Mgeni rasmi Jaji Warioba akiwahutubia maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari kwenye ukumbi wa mbayuwayu (AICC) |
Mta mada juu ya ushuhuda Edwin Soko akiwasilisha mada katika maadhimisho hayo. |
WAANDISHI Nchini wametakiwa kutokata tamaa katafuta na kuripoti habari zao zenye ukweli kwa jamii ili kuchochoea maendeleo bila kuogopa vikwazo mbalimbali toka kwa dola ya Nchi.
Hayo yamesemwa leo na jaji mstaafu Mark Boman kwenye kilele cha maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yaliyofanyika jijini Arusha kwa kuwakutanisha zaidi ya waandishi wa habari 500.
Jaji Boman alisema kwa sasa waandishi lazima waongeze juhudi katika kazi zao bila kuogopa kutishwa au kusongwasongwa na watawala au kundi fulani la watu wenye kutaka maslahi yao yalindwe na kuwaumiza wengine walio wengi.
Aliongeza kuwa mwandishi lazima awe na uwezo wa kupata taarifa na kuzifanyia uchambuzi na kuzifikisha kwa jamii kwa muda mfupi na kuisaidia jamii kwa ujumla.
Maadhimisho hayo yalitanguliwa na uwasilishaji wa mada toka kwa wataalamu mbalimbali , zilizotoa mifano ya kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari Tanzania.
Pia baadhi ya waandishi walitoa ushuhuda kwa matatizo mbalimbali yaliyowapata wakati wakitekeleza kazi zao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.