Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam jana na Afisa Uhusiano na Matukio wa Kampuni ya Airtel Dangio Kaniki alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa wapiga picha wa habari kuwajengea
uwezo kufanya kazi katika mazingira hatarishi.
"Tutaendela kuwapatia mafunzo wapiga picha ili wapate ujuzi zaidi katika utendaji wao wa kazi kwa kuwa mabalozi wetu,na tutawatafutia vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufanyia kazi katika mazingira hatarishi"alisema Dangio
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Baraza la Habari (MCT),na kudhaminiwa na kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya MP5 2011 yanashirikisha wapiga picha kutoka magazeti na TV.
Akizungumza katika mafunzo hayo mshiriki Suleiman Mpochi ambae pia ni mratibu wa mafunzo hayo alisema watanufaika nayo kwa kuwa watajifunza mbinu mpya za kufanya kazi katika mazingira hatarishi pamoja na
kufuata maadili ya taaluma ya waandishi wa habari.
Kampuni hiyo ni mara ya tatu inadhamini mafunzo hayo kwa wapiga picha za habari ambamo Mwezeshaji katika mafunzo hayo Mkongwe wa Habari katika fani ya habari Ndimara Tegambwage aliiomba kampuni kuendela
kudhamini mafunzo hayo na kuwapatia zana za kisasa za kazi wapiga picha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.