Ni shehena ya magodoro imehifadhiwa katika kila stoo na kona zilizojificha kituoni hapa. |
Nyakati za usiku baadhi ya mapango la mabanda haya ya kuuzia vyakula hugeuka kuwa danguro na watu huja hapa kumaliza haja zao. |
Lundo la vitendea kazi limenaswa kituoni hapa. |
Seleka, kasheshe, mbinde. |
Hifadhi ya vitendea kazi. |
Mkuu wa mkoa Ndikilo kikazi zaidi. |
Meya Mabula kikazi zaidi. |
Mkurugenzi wa jiji kikazi zaidi. |
Wananchi wameitikia kwa dhati mpango huu wa usafi. |
Kikazi zaidi. |
Harambee. |
Vijana nao wako mbele kufanikisha. |
Zoezi lilikamilika kwa uchomaji wa taka hizo. |
HABARI KAMILI.
MPANGO wa usafi
umefumua gesti bubu na madangulo katika stendi ya Nyegezi jijini Mwanza.
Tukio hilo limetokea mwishoni
mwa juma lililopita wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, Meya
wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka
Konisaga, Mkurugenzi wa Jiji Alfa Hassan Hida na Diwani Dismas Masunu (Butimba) walikuwa katika zoezi la usafi jamii shirikishi katika maeneo ya Stendi hiyo.
Kufumuliwa kwa gesti hizo bubu katika majengo ya wasafiri, na katika baadhi ya majengo yanayotumiwa na mama lishe,
maduka na maofisi yaliyopo maeneo hayo kunafatia uchafu uliokuwa umekithili na
kusababisha Meya Mabula kuagiza wafanyabiashara katika stendi hiyo kufunga
kwanza biashara zao ili kushiriki katika zoezi hilo la usafi wa mazingira.
“Haiwezekani leo
viongozi tuje kufanya usafi ninyi mmekaa na kuendelea na shughuli zenu wakati
nyinyi ndo mnaozalisha takataka hizi, lakini hamna hata chembe ya aibu kuona
Mkuu wa Mkoa Ndikilo anafagia na kuzoa takataka hata bila kushituka mnaendelea
kusonga ugali na kupanga vitu maeneo yasiyoruhusiwa.
Kufuatia Hatua hiyo
Mkurugenzi Hida alimuamuru Mtendaji wa Kata Hiyo kuwataka wafanyabiashara wenye
vibanda ndani ya stendi hiyo kufunga mara moja na vingine kuondolewa kupisha
usafi kufanyika ili kuweka mazingira safi yanayolidhisha na kuwepo uhalisia wa
stendi ya mabasi na abiria wanaosubiria usafiri.
Aidha kutolewa kwa amri
hiyo kulizua mtafaruku kwa baadhi ya makundi ya vijana wanaodaiwa ni wapiga
debe na makuli wa kubeba mizigo kudai kwa kupaza sauti kuwa kuna watu wamegeuza
stendi kuwa madanguro na gesti bubu ndani ya majengo ya huduma za chakula na humo ndani kuna magodoro mengi kwaajili ya watu kumaliza haja zao.
Baada ya makelele hayo
Mkurugenzi Hida, Meya Mabula, Diwani Masunu, Mtendaji , Afisa Afya wa Jiji
Kamenya kuingia ndani ya majengo ya stendi kushuhudiwa kilichokuwa
kikilalamikiwa na vijana hao jambo ambalo lilimshangaza kila kiongozi na
wananchi wakiwemo wanafunzi wa chuo kikuu cha St. Agustine (SAUT) walioshiriki
zoezi la usafi wa mazingira maeneo ya stendi ya Nyegezi ambapo ni kutekeleza
mpango kabambe wa usafi kila jumamosi ya kwanza ya mwanzo wa mwezi.
Akizungumza na
wananchi, wapiga debe wa stendi na wafanyabiashara wa maeneo ya stendi Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza Ndikilo, aliwaagiza Mkuu wa Wilaya Konisaga, Meya Mabula,
Mkurugenzi wa Jiji Hida, Diwani wa Kata hiyo na Afisa afya kufanya uwajibikaji
na kurudi kuchunguza tuhuma zilizoelekezwa kwa watendaji wa serikali waliopo
eneo la stendi.
“Hapa kuna tatizo
haiwezekani mambo haya yanafanyika Mtendaji, Meneja wa stendi, Afisa afya wa
Kata, Mkuu wa Kituo cha Stendi hawatambui haya, hili haliwezekani naagiza
chukueni hatua kwa watendaji hawa na inawezekana stendi hii na mambo haya
kuachwa kufanyika ni mradi wa mtu na wanaficha wanajuwa” alisema
Aliongeza kwa kusema kuwa "Nawapa
wiki moja kuhakikisha hali ya usafi inarejea na kuhakikisha vibanda vyote
vilivyo kinyume cha utaratibu na sheria vinaondolewa na kuhakikisha haya
tuliyoyashuhudia leo yanakomeshwa na kutojirudia ikiwemo kuwachukulia hatua
kali viongozi watakashindwa kutekeleza majukumu yao"
Mhandisi Ndikilo
aliwataka wananchi na wadau mbalimbali kushiriki katika usafi na mazingira
katika maeneo yao ili kuendeleza juhudi zilizoanzishwa na uongozi wa Jiji hilo
la usafi ili kuhakikisha linaendelea kuwa safi na kuendela kushinda na kunyakua
tuzo ya usafi kwa mara ya tisa mfurulizo ikiwa ni kama utamaduni.
“Tujitokeze kutekeleza
mpango huu kwa vitendo na usafi iwe ni tabia na tuchukie uchafu kwani huleta
magonjwa ya kuambukiza kuharibu mazingira hivyo ni vyema tukaanza kuchukua
hatua za kuwachukulia hatua za kisheria wale wanaofanya uharibifu wa mazingira
kwa kutumia sheria ndogo za Jiji zilizopo kudhibiti hali hii” alisisitiza Mkuu
huyo.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Hida Hassan, tayari amewatangazia wafanyabiashara waliopo katika maeneo hayo ya stendi kuondoa
mabanda yaliyo kinyume cha utaratibu na sheria za mipango miji kwani kuachwa
wakifanya biashara kiholela kutasababisha kuendeleza uchafu kuzagaa kila kona hivyo kupoteza sifa na hadhi ya stendi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.