ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 25, 2014

PSPF YAKABIDHI COMPUTER 10 KUTATUA KERO ZA UKOSEFU WA VIFAA VYA TAALUMA CHUO CHA BUTIMBA.

Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa PSPF Adam Mayingu akizungumza na wahitimu wa Stashahada ya ualimu katika chuo cha ualimu Butimba (TTC) kilichopo mkoani Mwanza mkurugenzi huyo vilevile amewashauri wahitimu wa fani hiyo kujiunga na mifuko ya hidadhi ya jamii ili waweze kujiwekea akiba ya baadaye.
"Utendaji wa sasa unaohitajika kwa sasa ni ule unaozingatia utaalamu, mnatakiwa muwe wabunifu mfuate sheria na taratibu mbalimbali zinazo ongoza kada hii ya ualimu" alisema Mayingu.
Wahitimu wa chuo cha Ualimu Butimba jijini Mwanza wakiwa wamebeba Computer zipatazo kumi walizokabidhiwa na Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa PSPF Adam Mayingu ikiwa ni mchango wa mfuko huo kwa kituo hicho cha elimu kukabiliana na changamoto ya vitendea kazi kwa mawasiliano.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa PSPF Adam Mayingu (wanne kutoka kulia) akikabidhi Mkuu wa chuo cha ualimu Butimba John Moleli  Computer 10, zitumike kukabiliana na changamoto ya vitendea kazi kwa mawasiliano.
Mkuu wa chuo cha ualimu Butimba John Moleli akizungumza na umma uliofurika kwenye maafali ya 79 ya Chuo cha Ualimu Butimba mkoani  Mwanza, ambapo jumla ya wahitimu 350 wakiwa ni walimu wa sayansi, Michezo, sanaa na maigizo pamoja na Sayansi jamii wamehitimu katika chuo hiki. 
Risala ya wahitimu.
Wanafunzi wa moja ya shule za msingi katika la jirani wakishiriki kusherehesha kusanyiko la maafali ya 79 Chuo cha Ualimu Butimba.
Ndani ya Chuo cha Ualimu Butimba kuna fani mbalimbali na hapa sanaa ilikuwa ikionyeshwa kama sehemu ya burudani.
Uwasilishaji kama ada na tamaduni.
Waalimu wahitimu wa fani ya Sanaa, Michezona Maigizo waliketi hapa
Waalimu wahitimu wa Sayansi waliketi hapa.
Walimu wahitimu wa Sayansi jamii walimu wa Art waliketi hapa.
Ni msafara wa wahitimu.
Muonekano toka pande hii.
Parade la wahitimu.
Wanasa matukio tukioni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.