Mjumbe wa Kamati kuu CCM Taifa Jerry Silaa (Meya wa Manispaa ya Ilala) akizungumza wakati wa kuwasimika Makamanda wa UVCCM Wilaya ya Ilemela jijini mwanza. |
Kamanda mteule wa UVCCM Abubakar Francis akikabidhiwa dhana za jadi za ulinzi na Jerry Silaa wakati alipomsika ukamanda kwenye uwanja wa Magomeni Kirumba. |
Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Jerry Silaa akimvika Barnabas Mathayo Joho la Naibu Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Ilemela |
Naibu Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Ilemela Barnabas Mathayo akiwapungia wananchi na wanachama wa CCM baada ya kusimikwa na Jerry Silaa Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa. |
Jerry Silaa akimshuhudia Barnabas Mathayo akila kiapo cha kuitumikia Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Ilemela kwa cheo cha Naibu Kamanda wa Vijana. |
"Pokea cheti cha shukurani kutambua mchango wako kutoka kwa UVCCM Wilaya ya Ilemela" akikabidhiwa na Jerry Silaa ni Barnabas Mathayo. |
Mwenyekiti wa wanawake wa Kikundi cha wauza samaki cha genge la Kabuhoro Kirumba akipokea shilingi milioni 1 zilizotolewa na Jerry Silaa (500,000) na Barnabas Mathayo (500,000) . |
Vijana wa Alaiki wakiwa katika utambulisho wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. |
Chipukizi wakiwa kazini |
Ilikuwa Burudani kubwa meza kuu walifurahia chipukizi wakitoa burudani. |
Wanachama wakisikiliza kwa umakini hotuba za viongozi meza kuu. |
Uzinduzi wa Shina la Vijana wakereketwa wa CCM Mtaa wa Kirumba Sokoni . |
Picha ya Pamoja Jerry Silaa na Makamanda wateule wa Wilaya na Kata tisa za Ilemela. |
MWANZA.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry Silaa,
amewatangazia kipigo cha mvua ya mawe, wabunge wenye ‘CV za porojo na ahadi
hewa’ wa majimbo ya Ilemela, Nyamagana na Ukerewe.
Alitangaza kipigo hicho wakati akisimika makamanda
wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Ilemela, mwishoni mwa wiki kwenye
uwanja wa Magomeni, Kata ya Kirumba jijini Mwanza.
Makanda waliosimikwa ni Abubakar Francis (Kamanda
mkuu wa wilaya), Barnabas Mathayo (Naibu Kamnda Mkuu wa wilaya) na wengine tisa
wa Kata za, Pasiansi, Kirumba, Nyamanoro, Sangabuye, Bugogwa, Ilemela,
Kitangiri, Nyakato na Buswelu.
“Msichague tena viongozi wanaotafuta CV kama wabunge
wa Ilemela, Ukerewe na Nyamagana wenye CV za porojo na uongo. Natangaza rasmi
kuwa majimbo haya tunayataka 2015 tuwatumikie wananchi.” Alisema Silaa na kushangiliwa
na umati mkubwa uliohudhuria sherehe za kusimikwa kwa makamanda hao.
Alidai kuwa, kila sinema huanza trela na dalili ya
mvua ni mawingu, CCM imeonyesha trela kuanzia kwenye chaguzi ndogo za Kata 27,
jimbo moja la Zanzibar, Kalenga na Chalinze hivyo wabunge Salvatory machemuli
(Ukerewe) Ezekia Wenje (Nyamagana) na Highness Kiwia (Ilemela) wajiandae kipigo
cha mvua yam awe kinakuja 2015.
“Wana CCM kufanya kosa siyo kosa kuliko kurudia
kosa. Huu siyo wakati wa kulaumiana bali ni wakati wa kushikamana na kwa kuwa
wabunga hawa wameanika ‘mahindi na mpunga’ nje wambienbi wajiandae kuuzoa kabla
ya mvua inayokuja wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao.” Alitamba.
Akizungumzia mchakato wa Bunge la Katiba
linaloendelea mjini Dodoma, Silaa alisema watanzania wengi ni wanyonge
wanahitaji muundo wa serikali mbili ambazo zitatumia rasilimali zilizopo kuwakwamua
kwenye umasikini na siyo serikali tatu ambazo zitawaongezea mzigo wa umasikini
na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
“Hakuna serikali yoyote ambayo haina gharama hivyo
wingi wa serikali ni mzigo kwa wananchi. Wanaong’ang’ania serikali tatu
wanataka kuwabebesha mzigo wa bure wananchi.” Alieleza.
Akizungumza kwa niaba ya makamanda wenzake
waliosimikwa, Mathayo safari ya ushindi wa CCM wilayani Ilemela imeanza kwa
kusimika kwao hivyo vijana wasikalie kulalamika, waungane kuwaondoa wabunge
wanaotumika matumbo yao badala ya weananchi.
“Kazi yetu kubwa sasa ni kuwaunganisha watu kisiasa
na kiuchumi. Kwakuwa mimi na CCM siyo wa longolongo kama wenzetu wa Chadema,
nawapa mtaji wa sh 500,000/= akina mama wa genge la samaki la Kabuhoro, naomba
mgeni rasmi mheshimiwa Silaa naye awaongeze.” Alieleza Mathayo.
Umati huo ulizizima kwa shangwe na vigelegele vya
akina mama Silaa alipowaongeza sh 500,000/= na kuwafanya wajipatie kitita cha
sh Milioni 1 huku akiwasisitiza akina mama na vijana wajiunge kwenye vikundi
vya uzarishaji mali Chama kiwawezeshe.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.