ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 30, 2014

AIRTEL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA OFISI KWA SHULE YA MSINGI CHAU CHALINZE.

Airtel Afisa mauzo wa kanda ya Pwani  William Mrocky akikabithi kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chau Bwana Elvin Msangi msaada wa viti na meza kwaajili ya ofisi ya walimu wa shule ya msingi ya chau iliyoko Chalinze Mkoani Pwani.
Airtel Afisa mauzo wa kanda ya Pwani  William Mrocky akikabithi kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chau Bwana Elvin Msangi msaada wa viti na meza kwaajili ya ofisi ya walimu wa shule ya msingi ya chau iliyoko Chalinze Mkoani Pwani.
Airtel yatoa msaada wa vifaa vya ofisi kwa shule ya Msingi  Chau Chalinze
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kwa kupitia shughuli zake za huduma kwa jamii imetoa msaada vifaa kwa ajili ya ofisi ya  walimu kwa shule ya msingi ya Chau iliyoko Chalinze mkoani Pwani.

Akiongea kwa niaba ya Airtel Afisa mauzo wa kanda ya Pwani  William Mrocky alisema” leo tunayofuraha kutoa msaada wa viti na meza kwaajili ya ofisi ya walimu shuleni hapa, msaada huu unalenga katika kuboresha mazingira ya ofisi  na kuwawezesha walimu kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Huu ni mwendelezo wetu wa huduma kwa jamii hususani katika sekta ya elimu ambapo kupitia mradi wetu wa “shule yetu” tumeziwezesha shule mbalimbali za sekondari kupata vitabu vya ada na kiada na kukabili changamoto za uhaba wa vitabu mashuleni. Sambamba na vitabu pia tunatoa msaada wa madawati na vifaa vya ofisi kama tunavyofanya leo katika shule hii ya msingi Chau.

”Tunaamini msaada huu utaleta tija na kuboresha utendaji wa kazi kwa walimu shuleni hapa” aliongeza Mrocky.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chau bwana Elvin Msangi alisema” nashukuru sana Airtel kwa kutufikia shuleni hapa, hii ni mara yakwanza kupokea msada kama huu shuleni hapa hivyo tunajisikia faraja kuona kampuni kama ya Airtel inafanya kazi kubwa katika kusaidia sekta ya elimu. Tunayo mahitaji mengi hapa shuleni, Tunategemea huu ni mwanzo hivyo mtatumkumbuka katika program zetu itakayokuja  siku za usoni.

Msaada huu utawawezesha walimu kuwa na ofisi nzuri na kuwaboreshea mazingira yao ya kazi kuwa bora zaidi.

Airtel kupitia mradi wake wa shule yetu unaziwezesha shule mbalimbali nchini kufaidia na vitabu, zaidi ya shule 900 nchini zimefaidika na mradi huu mpaka sasa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.