ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 21, 2014

ZANTEL YAKABIDHI MAJAKETI 1800 YA KUAKISI MWANGA KWA MADEREVA WA PIKIPIKI MWANZA.

Afisa Masoko Kanda ya Ziwa Gerlard Lusingu akikabidhi msaada wa majaketi 1800 ya kuakisi mwanga (reflective bips) kwa Katibu wa Kamati ya usalama barabarani (RTO) Nuru Seleman ili awakabidhi uongozi wa Bodaboda ambao unautaratibu wa jinsi ya kugawa kwa washirika wake wa vituombalimbali.
Wadau wakishusha maboxi yaliyobeba msaada huo wa majaketi kwa madereva wa bodaboda.
kisha ulihifadhiwa kwa muda katika stoo za jeshi la polisi mkoa wa Mwanza ili zipate kuandikwa namba pamoja na vituo vya watoaji huduma za usafiri wa pikipiki.
Katibu wa Kamati ya usalama barabarani (RTO) Nuru Seleman akizungumza na waandishi wa habari.
MOJA kati ya changamoto kubwa ambazo jeshi la polisi linakumbana nazo ni kusimamia sheria za usalama barabarani kuhusiana na uendeshaji wa pikipiki ambao umekuja kwa kasi na changamoto zake na moja kati ya changamoto kubwa ni kwamba madereva wengi wamekuwa ni wale wasiopitia mafunzo maalum ya uendeshaji zaidi ya kujifunza mitaani na kuingia kwenye biashara ya utoaji huduma ambapo hawa wamekuwa chanzo cha ajali nyingi.

"Ikumbukwe kuwa moja kati ya ongezeko kubwa la ajali hasa nyakati za usiku ukiachilia mbali aina ya uendeshaji wa dereva vilevile uonekano hafifu wa mwonekano wa chombo ilikuwa changamoto kubwa sana  ambayo imechangia ongezeko la ajali nichukuwe nafasi hii kuwapongeza Zantel kwa hatua hii waliyoifanya ni yangu matumaini watarudi tena na kuliwezesha kundi jingine lililobaki ili kuwafikia madereva wapatao elfu kumi wa mkoa wa Mwanza" alisema RTO.

Takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2012 jumla ya ajali 169 za pikipiki zilijitokeza. Kwa mwaka 2013 jumla ya ajali 89 za pikipiki hili ni punguzo la asilimia 34 ikiwa ni jitihada za kamati ya usalama wa barabarani na wadau wenyewe kuitikia wito wa kupata elimu ya usalama barabarani.
Afisa Masoko Kanda ya Ziwa Gerlard Lusingu.
"Pamoja na kutoa huduma ya mawasiliano kwa simu za mkononi Kampuni ya Zantel, haiko radhi kuona jamii ya watanzania ambao ni watumiaji wa huduma yake wakipoteza uhai kutokana na uzembe na udhaaifu wa mapungufu ambao yanaweza kudhibitiwa hivyo tulipo pokea ombi kutoka kamati ya usalama barabarani hatukusita kutimiza hilo nasi twajivunia kwani huu ni mwanzo tu tutarejea tena" alisema Lusingu

Mwenyekiti wa waendesha Bodaboda mkoa wa Mwanza, Makoye Kayanda akionyesha sehemu ya msaada wa majaketi 1800 ya kuakisi mwanga (reflective bips).
Mwenyekiti wa waendesha Bodaboda mkoa wa Mwanza, Makoye Kayanda akitoa shukurani zake kwa Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Zantel Tanzania kwa msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 11. Utaratibu wa ugawaji utakuwa ni kituo kwa kituo ambapo uongozi utakutana na viongozi wa vituo hivyo nao kutoa orodha ya waendeshaji bodaboda wa vituo husika ambao watagawiwa kwa namba na kuandikishwa kwenye daftari la usajili.
Baadhi ya madereva wa bodaboda waliowakilisha madereva wa mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya majaketi 1800 ya kuakisi mwanga kwa aajili ya uonekano maradufu nyakati za usiku.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.