Hili ni sehemu ya kusanyiko la baadhi ya wanafunzi wa Shule ya sekondari Magu waliohudhuria makabidhiano hayo. |
"Msaada wa Fedha tuliopokea ni huu" Mkuu wa Shule ya sekondari Magu Mwl. Geoffrey Mikenze (kulia) akiwa na wanafunzi wake. |
Serikali ya wanafunzi Shule ya sekondari Magu. |
Aksante.... |
MAGU.
KAMPUNI ya Lugumi
Enterprises Ltd & Ran It Solution imedhamilia kumaliza kero ya muda mrefu ya
ukosefu wa maji safi na salama katika Shule ya Sekondari ya Magu baada ya kutoa
msaada wa Pampu mpya ya kusukuma maji ili kukabiliana na kumaliza kabisa kero
hiyo Wilayani hapa.
Pamoja na msaada huo Kampuni hiyo pia imetoa kiasi
cha fedha shilingi milioni 10 tasilimu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo
la nyumba ya walimu familia mbili (two in one) ambalo lilishindwa kukamilika
kutokana na kukosekana fedha jambo ambalo sasa litakamilishwa na fedha
zilizotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo iliyo na tawi lake jijini
Mwanza.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi Pampu
hiyo na kiasi hicho cha fedha katika viwanja vya shule hiyo Mjini Magu jana, Meneja
wa Kampuni hiyo Eligod Sangawe aliyemwakilisha
Mkurugenzi wake Bw. Said Lugumi alisema kwamba utekelezaji wa msaada huo
unatokana na ombi la wanafunzi na walimu wa shule hiyo wakati wa sherehe za
Mahafali ya 24 ya 2013 kuwaaga wahitimu wa kidato cha nne kwenye risala yao kwa
Mgeni rasmi siku hiyo.
Sangawe alisema lengo kubwa ni kuhakikisha ukarabati
na miundombinu ya kufikisha maji shuleni hapo inaimarishwa na kuwezesha maji
safi na salama yanapatikana ili kuondoa adha ya kero ya muda mrefu iliyopo
katika baadhi ya maeneo ya Mji wa Magu ikiwemo Sekondari hiyo jambo ambalo
litawapatia fursa wanafunzi takribani 1,100 waliopo shuleni hapo kutumia muda mwingi katika masomo.
“Jitihada hizi zitasisimua mwamko wa jamii na wadau wengine wa elimu kuona kwamba wanayo nafasi ya kuchangia na kusukuma mbele gurudumu la elimu hapa nchini, hivyo sisi Lugumi Enterprises Ltd & Ran It
Solution tunayo matumaini kuwa msaada huu utatatua suala la mahitaji ya maji kwa asilimia 75 huku ule wa kompyuta utawasaidia kukimbizanana na mapinduzi ya Teknohama kutoka mfumo wa analojia na kuingia kwenye mfumo wa kidigitali"
Meneja Sangawe alisema kuwa kutokana na kuwepo
changamoto mbalimbali zinazoikabili sekondari hiyo, Kampuni hiyo hapo awali iliweza
kusaidia uboreshaji wa Maabara kwa kutoa vifaa ikiwemo Gesi na zana muhimu, kuboresha
mfumo wa maji wa maabara shuleni hapo pamoja na
kukabidhi Computer 3 za ofisi ikiwemo moja ya kufundishia masuala ya sayansi
na Teknohama.
Naye Mkuu wa Sekondari hiyo Geoffrey Mikenze
alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo na Meneja wake kwa kuamua kutoa
msaada huo italeta chachu ya mafanikio ya kielimu kwa shule yake.
“Kwenye risala yetu tulieleza kukabiliwa na
changamoto ya uhaba wa maji safi kwenye shule yetu, ukosefu wa rasilimali fedha
kwa ajili ya kukamilisha nyumba ya walimu yenye vyumba nane ikiwemo, sebule
mbili, stoo mbili (Two in One) Kampuni hii imetusaidia kiasi cha shilingi
milioni 10 ili kukamilisha wa ujenzi” alisema Mkuu huyo.
Ametoa wito kwa wadau mbalimbali wakiwemo
wafanyabiashara na wananchi ambao walipata kusoma katika sekondari hiyo kuiga
mfano ulionyeshwa na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Kizalendo ya Lugumi
Enterprises Ltd & Ran It Solution katika kusaidia kutatua changamoto
nyingine zilizobaki kama upungufu wa vitabu vya kiada na rejea, upungufu wa
matundu ya vyoo nane vya wavulana na vitano vya wasichana ili wanafunzi
kufaulu vyema na walimu kutoa taaluma bora.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.