ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 8, 2014

UTEGI FC NDIYO MABINGWA WA LAKAIRO CUP 2014.

Mabingwa wa michuano ya Lakairo Cup, Utegi Fc wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpambano wao na Nyanduga Fc ambapo walitwaa uchampioni kwa mikwaju ya penati 4-3, dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya 1-1.
Nyanduga Fc katika picha ya pamoja kabla ya fainali ya michuano ya Lakairo Cup iliyoenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 37 ya Chama cha mapinduzi (CCM), 
Mashabiki hawa wa liamua kuja na mwenge ambao inatajwa ulikuwa na kitu cha kamati ya ufundi siyo hivi hivi....
Tizama kwa umakini ni katikati ya uwanja njiwa mweupe alirushwa na wachezaji wa Utegi Fc kwaajili ya mamboz. ya neema.
Mashabiki wa Utegi Fc walikuwa wakishangilia mwanzo mwisho katika mchezo wa fainali baina ya timu yao na Nyanduga Fc ikiwa ni Fainali ya michuano ya Lakairo Cup iliyoenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 37 ya Chama cha mapinduzi (CCM).
Akina mama dimbani. 
Mchezaji wa Nyanduga Fc (red) akiruka juu sambamba na mchezaji wa Utegi Fc katika mchezo wa fainali ya michuano ya Lakairo Cup, Utegi Fc walitwaa uchampioni kwa mikwaju ya penati 4-3, dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya 1-1.
Vuta nikuvute.
Hapa waliketi mashabiki wa Nyanduga Fc. 
Mchezaji wa Nyanduga Fc akitolewa nje ya uwanja mara baada ya kufanyiwa madhambi katika mchezo wa fainali dhidi ya Utegi Fc.
Mashabiki wa Utegi Fc wakisherehekea ubingwa wao katika michuano ya Lakairo Cup, baada ya mchezo kuisha wakiibandua Nyanduga Fc katika penati 4-3, dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya 1-1.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rorya Mhe. Samwel Kiboye maarufu kama Namba 3 akitoa akizungumza na wananchi wa Kata ya Utegi wilayani Rorya ikiwa ni sambamba na kumkaribisha mgeni rasmi wa michuano ya Lakairo Cup iliyoenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 37 ya Chama cha mapinduzi (CCM), Mwenyekiti wa CCM mkoa mpya wa Geita Joseph Msukuma (katikati) huku mweyeji wa jimbo hili Mbunge wa Rorya Lameck Airo akisikiliza kwa makini kinachojiri.
Sehemu ya washiriki na wananchi na mashabiki walio hudhuria sherehe hizo.
Wachezaji wa timu ya Nyabikondo Fc wakisubiri zawadi zao mara baada ya kuikosa nafasi ya tatu nao kuambulia nafasi ya nne.
Kaptein wa timu ya Alonga Fc akiwa na zawadi ya shilingi milioni mbili aliyoipokea kwaniaba ya timu yake baada ya kuinyakua nafasi ya tatu michuano ya Lakairo Cup mchezo wa awali kusaka nafasi ya tatu katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kogalo Utegi wilayani Rorya mkoani Mara ambapo hadi mwisho Alonga Fc walinyuka Nyabikondo Fc bao 2-1 na kutawazwa washind
Kapteni wa Nyanduga Fc akiwa na kitita cha shilingi milioni tatu zawadi mshindi wa pili . 
Wachezaji wa Utegi Fc wakiwa na zawadi zao za ubingwa, kitita cha shilingi milioni 5, na mipira miwili. 
Mashabiki wa Utegi Fc na shangwe zao. 
Mwisho wa kabisa Mbunge wa Jimbo la Rorya Mhe. Lameck Airo alizungumza na wanahabari kuhusu lengo la michuano ya Lakairo Cup.Michuano ya Lakairo Cup 2014 ilishirikisha jumla ya timu 140, ikifanyika ndani ya miezi mitatu ikwa na malengo ya kuwafanya vijana kuwa bize na shughuli za kufanya ili kuwaondoa vijiweni sambamba na kuwaepusha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na uzinzi hatua ambazo kwa kiwango kikubwa zimefanikiwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.