ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 29, 2014

KAMPUNI YA REX ENERGY YATAMBULISHA TEKNOLOJIA MPYA YA KUHIFADHI NA KUSAMBAZA UMEME.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kusambaza vifaa vya umeme wa jua (solar) ya Rex Energy Bw Francis Kibhisa akizungumza na Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),kuhusiana na uzinduzi na utambulisho wa teknolojia  mpya yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kusambaza Umeme,mkutano huo umefanyika mapema leo asubuhi kwenye makao makuu ya ofisi hizo zilizopo mtaa wa Makamba,Gerezani jijini Dar.
Pichani mbele kushoto ni Ofisa Mauzo wa kampuni ya Rex Energy,Bwa.Medard Rweikiza pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Bwa.Francis Kibhisa wakiwaonesha na kuwaeleza baadhi ya Waandishi wa Habari namna moja ya kifaa cha kisasa kabisa chenye uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia Mwanga wa Jua (Solar).Kwa habari zaidi ingia www.rexsolarenergy.com
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy,Bwa.Francis Kibhisa akitoa ufafanuzi wa namna moja ya kifaa (pichani),kinachotumia teknolojia ya kisasa katika suala zima la kuzalisha umeme kwa kutumia mwanga wa jua (Solar Power) mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),Bwa.Francis alibainisha kuwa kifaa hicho kina uwezo wa kuwasha vifaa vya ndani kama vile taa,redio, friji, TV kwa wakati mmoja,na huuzwa kwa gharama nafuu.Pichani kulia ni Ofisa Mauzo wa kampuni ya Rex Enegy,Bwa.Medard Rweikiza akisikiliza
Baadhi ya  Wafanyakazi wa Kampuni ya Rex Energy wakiwa katika picha ya pamoja mara baada kumaliza mkutano wao na Waandishi wa habari mapema leo asubuhi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.