Afisa Habari wa Taasisi ya Sayansi Jamii (TASAJA) Bituro Kazeri (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo. |
TAMASHA la Utamaduni wa ngoma za asili kufanyika kesho kwenye uwanja wa michezo wa Nyamagana wakati familia na wananchi kutoka maeneo mbalimbali Mkoani hapa, watapata furusa ya kusherekea sikuuu ya mwaka mpya 2014 kwa burudani ya ngoma za asili kutoka makablia tofauti Jijini Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini hapa, Afisa Habari wa Taasisi ya Sayansi Jamii (TASAJA) Bituro Kazeri alisema kuwa kutokana na kujishughulisha na mambo yanayohusu jamii imeona umuhimu wa kuandaa tamasha hilo ili kuwapatia watoto nafasi ya kujifunza utamaduni wa ngoma za asili na kuendeleza mila na destuli za utamatuni huo.
Kazeri alisema kwamba taasisi hiyo imekuwa ikifanya shughuli za jamii na kuendeleza utamaduni wa ngoma za asili kutoka makabila mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza ili kuwapatia nafasi vizazi vijavyo kutambua na kushiriki kikamilifu kuuenzi kwa vitendo pamoja na kudumisha mila za makabira yao badala ya kupata historia tu ya utamaduni huo bila kuona njinsi ulivyokuwa kabla yao.
“Asili ya utamaduni wetu ni vyema ikadumishwa kizazi baada ya kizazi ikiwa na uaasilia kutoka tamaduni zetu tulizo rithi, hivyo basi ili tuweze kufikia malengo tunahitaji kukikuza kizazi cha sasa kwa mila na utamaduni endelevu kupitia ngoma za asili na kupata elimu ya historia ya makabila mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza na Kanda ya ziwa nay ale ya mikoa mingine nchini kwa ujumila” alisema.
Aidha Kazeri alieleza kuwa Taasisi hiyo inayoundwa na wahitimu wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini waliopata Elimu ya Sayansi Jamii kikiwemo cha SAUT cha Jijini Mwanza, ambao wamekuwa wakiamini masuala ya Sayansi ya jamii ni kuihusisha jamii na kutoa elimu na historia na vitendo ambavyo vitalenga kuendeleza mila na kuzidumisha kwa ngoma za asili na mambo mengine.
“Ukiacha ngoma zinazochezwa wakati wa Bulabo, mashindano ya Balimi na sherehe za serikali, tumeamua kuweka utaratibu wa ngoma hizi kwa kwenda maeneo mbalimbali na kushirikisha vikundi vya ngoma za asili za makabila ya mkoa wetu na kanda ya ziwa kwa lengo la kuhamasisha jamii kuuenzi na kuwapatia wananchi burudani hii” alisema Afisa huyo.
Aliongeza kuwa katika tamasha hilo lililobeba kauli mbiu ya Watoto Mwaka mpya Coca Cola na Utamaduni litawezesha vikundi vya ngoma za asili vya Mwanalyatu “hucheza na nyoka” kutoka Wilaya ya Magu (Mabingwa wa Mkoa huu), ngoma ya Utandawazi kutoka Wilaya ya Ukerewe (Washindi wa Pili Mkoa huu), ngoma ya Dogori ya Ukerewe, ngoma Sumbugu kutoka Wilayani Misungwi na Ritungu (Tarime).
Ametoa wito kwa wananchi wa Jiji la Mwanza kufika kujionea mabingwa na wataalamu wa kupiga ngoma kubwa, kucheza na nyoka, kucheza dogori na kujionea watoto wawili mabingwa wa ngoma toka ngoma ya utandawazi ya Ukerewe na ngoma maarufu ya Ritungu kutoka Mkoani Mara ambapo kuingia mlangoni kutakuwa na kingilio cha shilingi 1,000/= kwa watoto na 2000/= wakubwa usalama ni asilimia 100.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.