ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 31, 2013

ELIMU, GHARAMA ZA KUBWA ZA KUNUNUA MASHINE CHANZO CHA MGOMO WAFANYABIASHARA MWANZA.

Afisa habari wa Taasisi ya Sayansi Jamii (TASAJA) Bituro Kazeri akizungumzia sakata hilo mbele ya waandishi wa habari leo.
Na Peter Fabian wa G.Sengo Blog.
TAASISI ya Sayansi Jamii (TASAJA) mgomo si njia ya kumaliza tatizo la mashine za kutolea Ankala za (EFD) zinazotakiwa kuanza kutumika kuanzia January Mosi kwa utaratibu uliowekwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) unaoendelea toka jana Jijini Mwanza.

Akizungumza na vyombo vya Habari leo Jijini hapa, Afisa habari wa Taasisi hiyo Bituro Kazeri alisema kwamba kufatia mgomo baridi unaoendelea wa wafanyabiashara wa maduka makubwa ya kati na rejareja kupinga kupatiwa mashine za kutolea ankala za mauzo ya bidhaa wanazouza kwa wateja kwa madai kuwa bei yake ni kubwa kuliko uwezo wa wawafanyabiashara hao jambo limeleta sitofahamu kwa wananchi.

Kazeri ameeleza kuwa kutokana na mgomo huo kuingia siku ya pili leo, taasisi hiyo imekugwa na imeamua kutoa tamko lake, taasisi hii ambayo imeanzishwa na Wahitimu wa  Vyuo vikuu nchini waliosoma Elimu ya Sayansi Jamii ambayo inajihusisha na masuala yanayohusu jamii, hivyo kuguswa na kuchukua hatua za kuitaka serikali na wafanyabiashara hao kuketi meza moja kwa mazungumzo ili kurejesha huduma kwa wananchi.

“Wafanyabiashara ni sehemu ya jamii na muhimu kwa usitawi wa nchi yetu, kuendelea kuwepo kwa mgomo huo unaosababishwa na kundi mojawapo ikiwa ni wafanyabiashara, serikali na chombo cha kukusanya Kodi kunaweza kukaathili jamii kwa kiwango kikubwa kupata huduma na mahitaji mhimu, ni vyema kukatumika taratibu na malidhiano yatakayomaliza mgomo huo kwa njia ya mazungumzo kwenye meza” alisema.

Afisa habari huyo alisema, Taasisi hiyo muhimu ya masuala ya jamii inaona ni vyema sasa Serikali ikatoa Elimu kwanza pili ikakubali kuchukua mzigo wa kugharamia mashine hizo kupitia mashirika ya fedha ya kimataifa kupata mikopo ikiwemo Benki ya Dunia na mashirika mengine yanayojihusisha na masuala ya fedha ili serikali iweze kuzitoa mashine hizo kwa wafanyabiashara kwa gharama nafuu zaidi ambazo zitarejeshwa kidogokidogo hadi kumaliza deni.

“ Mfano mzuri TRA itoe mshine hizo za EFD kwa wafanyabiashara kama Makampuni ya kutengeneza vinywaji baridi ya Coca Cola, PEPSI, TBL na SBL ambayo yanawagawia wateja wake Friji na kuwataka kununua bidhaa za Makampuni hayo kwa taratibu na mikataba waliyokubaliana, jambo ambalo hili likifanya na TRA kuwapatia wafanyabiashara hao kwa bei ndogo zaidi basi wanaweza kurudisha garama hizo kidogo wakati wa kupeleka mapato ya kila mwezi” alieleza.
Eneo la maduka pembezoni mwa Salmacone Mwanza.

Taasisi hiyo inatoa wito kwa wafanyabiashara wasiokuwa na tatizo la mashine hizo kuendelea kutoa huduma kwa wananchi na kwani TRA imekwisha warudishi fedha zao walizokwisha toa kulipia mashine hizo za Ankala na kuwataka wafanyabiashara wanaopinga kutumia wakae meza ya mazungumzo na viongozi wa Serikali, TRA na wadau wengine kumaliza tatizo lililopo badala ya kuzuia huduma kwa wengine kuendelea kutoa.

“Mgomo huu usiingiliwe na wanasiasa na baadhi ya kundi la watu wachache wanaotaka kutumia kivuli cha mashine za EFD kutekeleza majukumu yao kwa kisingizio cha kuhamasisha mgomo huku wanapotakiwa kukaa kwa pamoja kwa ajili ya mazungumzo kukataa na kuanza kutoa mashariti ya siyiyokuwa na hata chembe ya tija huku pia wakitoa vitisho vya kuchoma moto” alisema Kazeri.

Aliongeza kuwa ni uoga tu uliopo juu ya utumiaji wa mashine hizo lakini kimsingi teknolojia hii ya mashine ambayo hutumika duniani kote kukusanya Kodi na itawezesha na kurahishia TRA kukadilia mapato kwa mfanyabiashara atakayekuwa yuko registard kutumia mashine hizo na itaondoa ukwepaji wa kodi na siyo dhuma na unyonyaji wa mapato hivyo ni vyema ikaondolewa hofu hiyo na kwa Sayansi ya Teknolojia na hoja ya wafanyabiasha kimsingi ni nzuri lakini mwisho wa yote ni lazima kulipa mapato.

Ameitaka serikali pia kuwa makini na watu ambao wamekuwa wakijipa vyeo vya kuongoza makundi ya kijamii na kutoa matamko mbalimbali kwa kuwatambua na kujua uhalali wao katika makundi wanayowawakilisha ili kudhibiti nchi hii kuwa na watu wanaojiamlia na kufanya mambo yasiolitakia mema taifa letu na wananchi kwa ujumla kwa kuchukua hatua na kutumia sheria zilizopo.

Maduka ya mitaa yote ya mitaa muhimu katikati ya jijini Mwanza yamepigwa kufuli na wamiliki wake kujipa mapumziko ya muda usiojulikana kutokana na mgomo unaoendelea.
Kuelekea Pangani Music Centre.
Kwa Mukpar.


Ofisi za huduma za utalii.
Barabara ya Nyerere.
Food Square na jengo la Toto.
Kuelekea Delux Night Club.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.