ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 18, 2013

TBL YASHEREHEKEA MIAKA 20 YA UBIA NA WASAUZ NA MIAKA 20 TANGU KUANZISHWA KIWANDA CHAKE MWANZA

Hizi ni shange za sherehe za miaka 20 ya ubia kati ya kampuni ya bia nchini Tanzania Breweries Limited (TBL) na Kampuni ya SB Miller pamoja na miaka 20 ya tangu kuanzishwa kwa kiwanda cha bia TBL Mwanza. Zaidi msikilize Richmond Raymond Meneja wa Kiwanda cha TBL Mwanza.

"Tunajivunia ubia wetu"
"Lete nyama choma tusherehekee kwa pamoja" 
Burudani ilihusishwa...
Haya twendeeee....!
Katika kusherehekea miaka 20 ya ubia na kuanzishwa kwa kiwanda cha TBL Mwanza, zawadi kwa wafanyakazi bora wa miezi mitatu mitatu zimetolewa nao wafanyakazi wakapata fursa ya kujumuika pamoja. 
Kuja kwa ubia kumeleta faida kubwa kwa jamii ikiwa ni sambamba na ajira kwa vijana wasomi wenye uwezo wa kufanya kazi.
Wadau wa ukweli katika wakifuatilia yanayojiri eneo la sherehe viwanja vya ndani vya kampuni ya bia vilivyopo Ilemela jijini Mwanza.
Meneja mauzo wa TBL Shinyanga Robert Kazinza (katikati) akiwa na wafanyakazi wenzake wa kampuni hiyo katika hafla fupi ya kusherehekea miaka 20 ya Ubia kati ya Kampuni ya bia nchini Tanzania Breweries Limited (TBL) na Kampuni ya SB Miller pamoja na miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kiwanda cha bia Mwanza.
"Tumeweza kutengeneza Kampuni kubwa ambayo imekuwa mlipa kodi mkubwa wa Serikali".
Katika kipindi cha ubia mapinduzi makubwa yaliyojitokeza yamesababisha ufanisi katika utendaji kazi ambao unaboreshwa sambamba na mabadiliko ya teknolojia, hivyo kuleta utofauti mkubwa kabla ya miaka 20 ya kuingia ubia. 
Wadau walisherehekea bila wasiwasi.
Katika kipindi chote TBL inajivunia ubora wa bidhaa zake,
 - Ufanisi wa huduma kwa wateja
- Kasi ya kuchangia uchumi wa Tanzania kupitia ulipaji kodi uliobreshwa kuliko Kampuni yoyote ile nchini.
- Kuongeza ajira nchini.
- Tumerejesha faida kwa jamii katika kuboresha huduma za Afya, Elimu, Mazingira, Kufadhili michezo, Huduma za maji na kadhalika.
Tabasamu la kujiamini....!!
hureeeee.....!!!
"Yep we are"
Burudani muhimu ya muziki wa kisasa.!
Live band.
Tunasisitiza chakula kwa afya. 
Haya tule...!!
"Kaka naomba pilipili..."
"Naanzia na hii"
Kilichomo sahanini...!
"Lete mzigo"

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.