MFUKO wa Pesheni wa PPF Kanda ya Ziwa imeyaonya baadhi
ya Makampuni mbalimbali yakiwemo ya Ulinzi kwa tabia na mazoea ya kuwaandikisha
wafanyakazi wao na kushindwa kuwasilisha michango yao hali inayopelekea
wafanyakazi kuangaika kupata fedha za michango waliyokuwa wakikatwa na kuchangiwa
na waajiri wao mara wanapotoka katika ajira.
Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Meshack
Bandawe Meneja wa Kanda ya Ziwa (PPF) alipokuwa mgeni rasmi wakati wa hafla
fupi ya kufunga mafunzo ya askari wa ulinzi 35 waliohitimu kati ya 40 Kampuni
ya K.K Security walioanza mafunzo hayo kwenye uwanja mkongwe wa michezo wa
Nyamagana jijini Mwanza. (ZAIDI BOFYA PLAY KUMSIKILIZA )
Bandawe alisema kuwa Kampuni ya K. K Security
imekuwa ikithamini shughuli za Mfuko wa Pesheni wa PPF kama mdau muhimu katika
sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa manufaa ya mwajiri na wafanyakazi kwa ujumla
katika kuwakinga na majanga mbalimbali wawapo katika ajira ama nje ya ajira.
Mkurugenzi huyo, alisema kwamba PPF imedhamilia
kutoa huduma bora kwa makampuni yanayo wasilisha michango yao kwa wakati huku baadhi
ya makampuni yanayoshindwa kufanya hivyo yatachukuliwa hatua kali za kisheria
ili kulinda maslahi ya wafanyakazi na katika kutekeleza hilo tayari Mfuko wa
PPF umekwisha yafungulia kesi Mahakamani baadhi ya makampuni ya ulinzi
yaliyoshindwa kutimiza wajibu wao.
Bandawe alisema kwamba baadhi ya makapuni yamekuwa
yakikumbwa na changamoto kubwa na kuibuka migogoro na wafanyakazi wao kutokana
na kuwalipa mishahara midogo , lakini mbaya zaidi mishahara hiyo midogo hailipwi
kwa muda na wakati hali hiyo inawafanya baadhi ya wafanyakazi wamekuwa na
maisha ya shida na familia zao huku wakikabiliwa kufanya kazi katika mazingira
magumu.
Mkurugenzi huyo aliipongeza Kampuni ya ulinzi ya
K.K.S kuwa mfano wa kuigwa na makapuni mengine nchini ambapo kumbukumbu
zilizopo zinaonyesha kuwa kampuni hiyo inajumla ya wafanyakazi 6285
walioandikishwa katika mfuko wa pesheni wa PPF na huwasilisha michango yao
isiyopungua kiasi cha shilingi milioni 267,771,967.00 kila mwezi katika ofisi
mbalimbali za PPF katika Kanda zote nchini.
Ukaguzi wa parade. |
PPF itaendelea kutoa mikopo ya gharama nafuu kupitia
SACOSS zilizopo kwenye sehemu za kazi pamoja na kushiriki katika ujenzi wa
nyumba za gharama nafuu zinazokopeshwa kwa wanachama wake ili kuwawezesha
kumiliki nyumba kabla ya kustaafu, PPF pia inawasii wafanyakazi wapya
watakaoajiriwa na makampuni na taasisi katika sekta ya umma , serikali kuu,
serikali za mitaa, binafisi na zisizo za kiserikali na isiyo rasmi kujiunga
wapate mafao bora na huduma bora zinazotolewa na Mfuko huo.
Kakakamavu wa wahitimu. |
Mguu sawa. |
Attention..! |
Namna ya kujilinda. |
Meza kuu ya wadau wa PPF na KK Security Mwanza. |
Kwa umakini yanayojiri uwanjani kutoka jukwaa kuu. |
Parade likitoa heshima kwa jukwaa kuu. |
Naye Meneja wa Tawi la Mwanza wa Kampuni ya K.K.S Bi. Levina Beal (pichani) alisema kuwa kutokana na askari walioajiriwa kukubali kukatwa asilimia 10 ya mishahara yao kumesaidia wao kupeleka michango ya asilimia 10 kama mwaajiri kutokana na sheria za mfuko huo zinavyoelekeza kwa wakati ili kuondoa malalamiko yanayojitokeza baada ya wafanyakazi kuacha au kutoka kazini ili kukwepa malimbikizo jambo ambalo wamekuwa wakilitekeleza kila mwezi. (ZAIDI BOFYA PLAY KUMSIKILIZA)
Beal alisema kuwa kutokana na Kampuni yake kuwekeza katika sekta ya ulinzi imeamua kutenga fedha kwa ajili ya kugharamia mafunzo kwa askari wake inaowaajiri ili kuwa na weledi wa ulinzi wenye kiwango kinachokubalika ikizingatiwa kuwa Jeshi la Polisi pekee haliwezi kumudu kufika kila mahali kuweka ulinzi na badala yake sekta binafisi imekuwa mdau wa kutoa ulinzi kwenye makampuni, taasisi za umma, mashirika ya umma na yasiyo ya serikali na watu binafisi hapa nchini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.