ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 13, 2013

MAAFALI YA 6 CHUO KIKUU CHA BUGANDO KUFANYIKA TAREHE 16 NOV 2013.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba ya Afya cha Bugando CUHAS) Prof. Jackob Mtabaji (kulia) akiwa na Naibu Makamu Mkuu wa Taaluma Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba ya Afya cha Bugando (CUHAS) Prof. William Mahalu wakati wakizungumza na waandishi wa habari wako katika picha zinazofuata kuhusiana na maafali ya 6 Chuo kikuu cha Bugando Mwanza.
CHUO kikuu cha sayansi na Tiba ya Afya cha Bugando Jumamosi ya tarehe 16 Novemba 2013 kitakuwa na maafali ya 6 tangu kuanzishwa kwake na maafali ya pili tangu kipate hadhi ya kuwa chuo kikuu kamili vilevile ni miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, kikiwa na lengo la kupunguza changamoto ya uhaba wa madaktari wenye sifa na wataalamu wa tiba nchini.

Zaidi msikilize Prof Mtabaji kwa kubofya play.
Chuo Kikuu cha Bugando kilianza na wanafunzi 10 na sasa kina wanafunzi 1,500. Ambapo jumla ya wanafunzi 1038 wanatarajiwa kuhitimu mwaka huu (tarehe 16 nov 2013).
Wanahabari wakichukuwa taarifa.
Kama ilivyoada maafali hayo yatatanguliwa na misa takatifu itakayoanza saa 2:30 na kabla ya hapo siku moja kabla ya tukio yaani ijumaa ya tarehe 15 kutakuwa na  mchezo wa mpira wa miguu kati ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Bugando na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT na kisha mchezo utakaofuata utakuwa baina ya Waalimu na wahitimu wa Chuo Kikuu Bugando, michezo yote ikichezwa dimba la CCM Kirumba Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.