TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Toleo la Leo
BALIMI EXTRA LAGER YATANGAZA RASMI UDHAMINI WA MASHINDANO YA MBIO ZA
MITUMBWI KANDA YA ZIWA KWA MWAKA 2013.
Dar es
Salaam, Jumatano 16 October 2013: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra leo
imetangaza rasmi kudhamini kwa mara nyingine tena mashindano ya mbio za
mitumbwi kwa wakazi wa kanda ya ziwa kwa mwaka huu 2013. Mashindano haya ya “kupiga makasia” yanafanyika kwa mwaka
wa kumi na nne mwaka huu na yamekuwa na hamasa na msisimko mkubwa kwa wakazi wa
maeneo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam
leo, Meneja Masoko wa kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) Bwana Fimbo Butallah alisema kwamba lengo hasa la Bia ya
Balimi Extra kudhamini mashindano haya ni kufurahi pamoja na wakazi wa kanda ya
ziwa hususani wale ambao ni wavuvi. Aliendelea kusema, “Mashindano haya
yanaenzi na kulinda tamaduni zetu zisipotee, yanajumuisha watu mbalimbali
kukutana, kufahamiana na kufurahi kwa pamoja na hii inasaidia sana kuimarisha
amani na upendo baina yetu. Amani ni nguzo muhimu sana kwa Taifa letu”.
Alisisitiza pia umuhimu wa michezo katika kujenga afya bora.
Bwana Fimbo alifafanua kwamba kwa mwaka huu mashindano ya
mitumbwi yatahusisha miji mitano ya kanda ya ziwa. Yataanza rasmi mchakato wake
Jumamosi hii tarehe 19 October katika mji wa Kigoma na kisha kuelekea mji wa
Bukoba katika mkoa wa Kagera. Yataendelea mjini Mwanza, kisha katika kisiwa cha
Ukerewe ambapo yatamalizikia katika mji wa Musoma. Washindi watakaopatikana
katika miji hii watashindanishwa kwa pamoja ili kumpata mshindi wa kanda.
Shindano la kumpata mshindi wa kanda linategemewa kufanyika jijini Mwanza
mwanzoni mwa mwezi December. Tarehe za mashindano haya ni kama ifuatavyo;
1. Mji wa
Kigoma; Jumamosi tarehe 19
October Ufukwe wa Kibirizi.
2. Mji wa
Bukoba; Jumamosi tarehe 02
November Ufukwe wa Spice Beach.
3. Mji wa
Mwanza; Jumamosi tarehe 09
November Ufukwe wa Mwaloni.
4. Kisiwa
cha Ukerewe; Jumamosi 16 November Ufukwe Hoteli ya
Monarch.
5. Mji wa
Musoma; Jumamosi tarehe 23
November Ufukwe wa Bwalo la Polisi.
6. Mashindano
ya Kanda; Jumamosi tarehe 07 Dec Ufukwe Mwaloni, Mwanza.
Bwana Fimbo akizungumzia zawadi za mwaka huu alisema kwamba
katika ngazi ya mikoa na ngazi ya kanda Balimi Extra imetenga zaidi ya shilingi
milioni ishirini na nne kama zawadi za pesa taslimu kwa washindi. Mpangilio wa
zawadi ni kama inavyoonekana hapa chini;
ZAWADI
|
NGAZI YA MKOA
WANAUME
|
NGAZI YA MKOA
WANAWAKE
|
NGAZI YA KANDA
WANAUME
|
NGAZI YA KANDA
WANAWAKE
|
Mshindi wa Kwanza
|
900,000
|
700,000
|
2,700,000
|
2,300,000
|
Mshindi wa Pili
|
700,000
|
600,000
|
2,300,000
|
1,700,000
|
Mshindi wa Tatu
|
500,000
|
400,000
|
1,700,000
|
900,000
|
Mshindi wa Nne
|
400,000
|
300,000
|
900,000
|
700,000
|
Mshindi wa 5 - 10
|
6 @
250,000
|
6 @
200,000
|
6 @
400,000
|
6 @ 250,000
|
Bwana Fimbo alimaliza kwa kuwaomba wanachi wa kanda ya
ziwa wajitokeze kwa wingi katika miji iliyotajwa ili kufurahi kwa pamoja katika
matamasha haya. Alisisitiza wasisahau mila na tamaduni zao katika kipindi
ambacho watu wengi hupenda kuiga tamaduni za kimagharibi. Alimaliza kwa
kuwashukuru sana wanywaji wa bia ya Balimi Extra kwa kuchagua bia hii na kuomba
waendelee kuitumia kwani ni kupitia mchango wao ndipo pia Balimi Extra Lager
inaweza kuleta burudani kama hizi kwa ajili yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.