Kabla ya mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa Taifa Simba na Azam FC wote walikuwa na pointi 20 sawa na Mbeya City wakitofautiana katika uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Simba walikuwa wa kwanza kuliona lango la Azam Fc katika dakika za kwanza za mchezo huo na alikuwa Ramadhani Singano ndiye aliyeifungia timu hiyo.
Kabla kipindi cha kwanza hakijamalizika Kipre Tchetche aliisawazia Azam Fc.
Kipindi cha pili katika dakika za lala kwa buriani alikuwa ni Kipre Tchetche tena ndiye aliyekomelea msumari wa mwisho kwa Simba na hatimaye mchezo ukashuhudia Azam ikiibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Wanamsimbazi (Simba) ambao kabla ya mchezo huo hawajawahi kupoteza mchezo zaidi ya kuambulia sare kwenye michezo yake kadhaa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.