ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 9, 2013

OFISI MPYA ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU KUZIPIGA BAO OFISI ZA JIJI LA MWANZA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Magu na Ukumbi wa Mikutano. Ofisi hizo za kisasa kulingana na michoro yake zitazidi uzuri na ubora wa zile za sasa za Halmashauri ya jiji la Mwanza. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injini a Evarist Ndikilo akishuhudia tukio hilo na kulia mwenye kipaza sauti ni Mkuu wa Wilaya hiyo Jaqueline Lianna.

Jiwe la msingi lililowekwa na Mhe. Rais Jk.

Rais Kikwete akipata maelezo toka kwa mtaalamu wa ramani namna jengo hilo litakavyokuwa pindi likikamilika.

Taswira ya majengo ya ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Magu na Ukumbi wa Mikutano.

Ujenzi huu umeanza katika mwaka wa fedha 2012-2013 unafanyika katika eneo la Ilungu kata ya Nyigogo, eneo la kilimeta saba kutoka Magu mjini na lina ukubwa wa hekta 4.3, ujenzi huu umekwenda sambamba na upimaji wa viwanja 800 katika eneo hilo ili kuleta taswira mpya ya mji mpya utakaojengwa.

Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuwataka wakandarasi hao kutimiza lengo lililowekwa kwa ujenzi huo kukamilika kwa ubora ulioelekezwa na kwa wakati.
Jumla ya shilingi milioni 380 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri zimelipwa kwa wananchi 373 ikiwa ni fidia ya ardhi na mali eneo la mradi lenye ukubwa wa ekari 480.

Aidha pamoja na fidia Halmashauri ya Wilaya imetoa kiwanja kimoja kwa kila mwananchi aliyekuwa na shamba katika eneo la mradi. 

Kisha shughuli ikahamia kwenye mkutano uliofanyika Magu mjini ambako maelfu ya wananchi walikuwa wakimsubiri kwa hamuRais wao.

Rais Kikwete akizungumza na wakazi wa wilaya ya Magu.

Utaratibu ulizingatiwa kusanyikoni hapa.

Waliokuwa mbali walitumia akili za ziada kushuhudia kilichokuwa kikijiri viwanjani hapa.

Mbunge wa Wilaya ya Magu Mhe. Festus Limbu akitoa maelezo juu ya changangamoto mbalimbali zinazoikabili wilaya hiyo pamoja na vijiji vyake katika sekta za Afya, Umeme na Maji, nyuma yake ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo ambaye ndiye alikuwa akiongoza mkutano huo kwa kuwakaribisha viongozi mbalimbali.

Mkurugenzi wa Idara ya Maji safi na maji taka mkoa wa Mwanza Anthony Sanga akitoa maelezo ya mikakati ya ofisi yake juu ya kukabiliana na suala la uhaba wa maji kwa wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza ikiwemo wilaya ya Magu ambapo Mh. Rais aliridhishwa na majibu yake.

Kusanyiko la wakazi wa Magu.

We ulikuwa wapi?

Rais Kikwete akimsikiliza kwa umakini mmoja kati ya wananchi wa wilaya ya Magu.

Wananchi wa Magu na hisia zao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.