ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 18, 2013

MRADI WA UJENZI WA DARAJA LA MONGOBHAKEMA KUSULUHISHA UTATA WA MAWASILIANO JIMBONI KISESA


Msimamizi wa ujenzi wa daraja la Mongobakima Injinia John akionyesha shughuli mbalimbali za ujenzi zinavyoendelea kwenye daraja hilo kubwa lililo muhimu lililopo katika jimbo la Kisesa mkoa mpya wa kisesa.
Mradi huo ulianza kutekelezwa mnamo mwezi march 2013 chini ya Mkandarasi aitwaye Passon Civil Contractors ambapo ujenzi haukuweza kuendelea kutokana na wingi wa maji, lakini mara baada ya maji hayo kupungua ujenzi ukaendelea. (Msikilize Injinia kwa kubofya play)
Katibu Mkuu wa CCM Abdalahman Kinana akiwa na mwenyeji wake Mbunge wa jimbo hilo la Kisesa Luhaga Mpina pamoja na viongozi wengine wakifanya ukaguzi wa daraja hilo lililo moja ya miradi inayotekelezwa chini ya Ilani ya Uchaguzi CCM ya mwaka 2010-2015.
Daraja hilo la Mongobakima litakuwa na urefu wa mita 32 likijengwa kwa kuunganisha barabara ya Mwabulutago - Mwasengela - Ngaka yenye urefu wa Kilomita 13.

Mradi mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi milioni 501,182,580 ikiwa ni fedha zilizokabidhiwa kutoka mfuko wa barabara.
Mafundi wakiendelea na kazi.

Katibu Mkuu wa CCM Abdalahman Kinana akisaini kitabu cha kuweka kumbukumbu wakati alipofanya ziara eneo hilo, pembeni (kushoto) ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Mhe. Titus Kamani.
Mradi ukikamilika utarahisisha matumizi ya barabara kupitika kirahisi kwa kipindi chote cha mwaka kwaajili ya kusafirisha mazao na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo suala la Afya, Biashara na Mawasiliano.
Nyenzo za ujenzi.

Kuelekea kule upande wa pili ni kijiji Mwabulutago na huku ni Mwasengela hadi Ngaka katika barabara yenye urefu wa Kilomita 13 kutoka vijiji na kata hizo.
Katapila likiendelea na kazi ujenzi wa daraja la Mongobakima.


Ziara ya Katibu Mkuu Mhe. Kinana ilipomalizika alisindikizwa na msafara hadi mto Simiyu ambako aliagana na mwenyeji wake Mbunge wa Kisesa Mhe. Luhaga Mpina (aliyeshikana mikono na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Nape Mnauye) 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.