ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 17, 2013

KINANA: MAWAZIRI TATUENI KERO ZA WANANCHI MOJA KWA MOJA: AVUTIWA NA UIMARA WA CHAMA JIMBO LA KISESA

Katibu Mkuu wa CCM (katikati ya umati) akipokelewa kwa maandamano na umati wa wakazi wa kijiji cha Mwasengela walioambatana na viongozi wao.

Kwenye kona kuelekea mkutanoni.

Katibu Mkuu wa CCM akipokelewa na umati wa wakazi wa kijiji cha Mwasengela huku akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo hilo (Kisesa) Mhe. Luhaga Mpina nyuma yake.

Ni mapokezi tu na shamrashamra kwa Katibu Mkuu wa CCM katika kijiji cha Mwasengela.
gz4
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka mawaziri husika kutatua kero za wananchi baada ya watendaji wa chini kushindwa kufanya kazi zao, alisema sasa baadhi ya watendaji wamegeuza kero za wananchi mitaji  na kuwachajisha pesa nyingi hasa wafugaji.
 Akihutubia wakazi wa kata ya Mwasengela alisema Mawaziri ni vyema sasa wakachukuwa jukumu la moja kwa moja kwenda kwenye maeneo ya wananchi na kutatua matatizo yaliyopo. 

Amesema wafugaji wa kata ya Mwasengela wamekuwa wakibughudhiwa na watu wa hifadhi ya Maswa  kupita kiasi kupitia sheria zisizozingatia wakati akizitaka baadhi ya sheria hizo zitizamwe kwani zinaweza zikawa zimepitwa na wakati hivyo ni vyema zikarekebishwa. (Bofya play kumsikiliza)


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya TLP lakini sasa amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi Zunzu Ndatulu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwasengela. Na hapa alikuwa akiwasilisha kero kuu ya wananchi kuhusu eneo la malisho.
Mwenyeji wa ujio huo Mbunge wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina akihutubia maelfu ya wakazi ya kata ya Mwasengela kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Ngoma iliyokuwa ikisikika hapa ilikuwa yaaina yake kiasi cha kuvunja rekodi ya ziara za kanda ya ziwa.

Diwani machachari anayekubalika wa kata husika almaarufu kwa jina la 'Darubini' akimwaga sera zake kwenye mkutano wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM. 

Sehemu ya umati uliofika kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mikoa mitatu ambapo jana alikuwa mkoani Simiyu na atamalizia mkoa wa Mara, tayari Katibu Mkuu ameshamaliza ziara ya mkoa wa Shinyanga na kuleta neema kwa wakulima wa pamba na wafugaji.

Mkuu wa Wilaya ya Meatu Rosemary Kirigini akisalimia wakazi wa kata ya Mwasengela wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihutubia.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa kata ya Mwasengela ambapo yupo kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mkoani   Simiyu .

Mwenyekiti wa CCM jimbo la Kisesa Dr. Kamani akimtambulisha aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya TLP lakini sasa amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi Zunzu Ndatulu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwasengela.

Wanachama 120 toka vyama mbalimbali wakiwa kwenye utambulisho wa kurudisha kadi za vyama vyao na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi. 

Wanachama 120 toka vyama mbalimbali wakiwa kwenye utambulisho wa kurudisha kadi za vyama vyao na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi. 

Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina akiwatambulisha wazazi wake kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi ilimchukua miezi mitatu kukubaliwa kwa ombi lake la kutaka kugombea ubunge jimboni kwake.

Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina akimtambulisha baba yake mzazi kwenye mkutano wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyofanywa na Katibu mkuu CCM Ndugu Kinana.

Kisha akahadithia jinsi alivyopata ugumu kukubaliwa na wazazi wake kuhusu suala la kugombea ubunge... (Bofya play kusikiliza)

Katibu Mwenezi wa Siasa CCM Nape Mnauye (Kushoto) aliingiwa hisia kwa kile kilichokuwa kikijili kwenye mkutano huo wakati Mbunge wa Jimbo la Kisesa akihutubia wananchi naye Katibu Mkuu CCM Abdarahiman Kinana akimsikiliza, kiasi kilichompelekea Mwenezi huyo kuchukua kamera kisha 'mwenyewe' kuzisaka engo muhimu kwa ajili ya kumbukumbu. 

Nao umati ulikuwa makini....

Wananchi wa kijiji cha Mwasengela.

Chifu Kilabanja Abdulrahman Kinana akiwaaga wakazi wa kata ya Mwasengela baada ya kumaliza Mkutano wa hadhara.
Fundi mitambo ni Francis Kaseko toka Shy Town alihakikisha kila kitu kinaenda smart. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na Mbunge wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina na wazazi wa mbunge huyo mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.